CHUO Kikuu Mzumbe kupitia kituo atamizi cha Vijana ambacho kinajishughulisha na kulea wajasiriamali mbalimbali wamekuja na mfumo wa ACOPONIC unaohusisha uzalishaji wa samaki pamoja na ulimaji wa mboga mboga bila kutumia mchanga.
Akizungumza jijini Dar Es Salaam leo, Mjasiriamali Kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Neslon Kisaanga wakati wa maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam amesema mfumo huo unamwezesha Mjasiriamali kufanya shughuli mbili kwa wakati mmoja.
"Mfumo huu unamtungi ambao unatumika kuzalishia samaki, lakini upande wa pembeni kunamabomba yanazungusha maji yanayosukumwa na mota kutoka kwenye mtungi wa kuzalishia samaki pia kuna makopo yaliyotobolewa kwaajili ya kupitisha hewa na kuvuta unyevunyevu, kwani mbegu, mche au mmea unaweza kustawi kupitia Unyevuvyevu unaopita kwenye haya mabomba." Amesema Kassanga
Kassanga amesema kuwa maji yanayopita kwenye mabomba ni kutoka kwenye mtungi wa kuzalishia samaki na kinyesi cha samaki kinatoa gesi ambayo inavirutubisho vingi vinavyoweza kukuza mmea na kuustawisha.
"Kwahi mfumo huu unapata faida mara mbili kwanza unapata Samaki kwaajili ya chakula lakini pia unapata mbogamboga ambazo ni nzuri kwaajili ya matumizi ya binadamu.
Mbali na hivyo kupitia mfumo huo wa ACOPONIC unasaidia kutengeneza Funza wanaopatikana katika matakataka hasa mabaki ya chakula kwahiyo taka hizo zinavyooza zinazalisha wadudu wanapitia hatua mbalimbali.
Amesema kuwa wadudu wanaozalishwa ni chakula cha samaki kwani wadudu hao wanaprotini nyingi lakini pia wadudu hao unaweza kulisha Nguruwe, bata na kuku.
Kassanga amesema lengo kuwa lengo la kutengeneza mfumo huo ni kupunguza taka kwenye mazingira pia wanatumia fursa zilizopo katika mazingira, badala ya kununua chakula kwaajili ya kulisha mifugo.
Hata hivyo amesema kuwa taka nyingi hutupwa lakini Chuo Kikuu Mzumbe kupitia kituo atamizi cha wajasiriamali wanaongeza mnyororo wa thamani ya kitu yaani Value Adition katika taka hizo.
"Kwahiyo unaweza kutumia taka zilizopo kwenye mazingira yako kuzibadilisha kuwa fursa na kujipatia kipato, kwahiyo katika mfumo huu unazalisha samaki, unazalisha mbogambona pia unaweza kufanya biashara nyingine ya kuzalisha wadudu kupitia takataka." Amesema Kassanga
Mfumo huo unaweza kuutengeneza katika eneo la wazi na katika ukubwa unaoutaka uwe mkubwa na wenye uwezo kiasi unachokitaka mtumiaji.
Hata hivyo Vijana wanaweza kutengeneza mfumo huo mahali popote kwani wamesha sajili kampuni yao Brela na mpaka sasa wanatoa huduma za kilimo pia wanaohitaji huduma hiyo, hivyo mwanamchi unaweza kuomba uangalizi kwaajili ya uwekaji mtambo huo kupitia chuo Kikuu Mzumbe Morogoro.
Mjasiriamali Kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Neslon Kisaanga akitoa maelezo kuhusu mfumo wa Acoponic wakati wa maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam yanayoendelea kufanyika.
Wanachi wakiangalia namna mfumo wa Acoponic unavyofanya kazi baada ya kupewa maelekezo na Mjasiriamali Kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Neslon Kisaanga wakati wa maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam
Mjasiriamali Kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Neslon Kisaanga akitoa maelezo kuhusu mfumo wa Acoponic wakati wa maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam yanayoendelea kufanyika.
Mjasiriamali Kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Neslon Kisaanga akimpa maelezo kuhusu mfumo wa Acoponic, Mkuu wa Kampasi ya Dar es Salaam Chuo Kikuu Mzumbe, Prefesa Honest Ngowi wakati wa maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam yanayoendelea kufanyika.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment