Naibu Waziri Nishati Mhe. Wakili.Stephen Byabato leo tarehe 08/07/2021amefanya uzinduzi wa Mradi wa kusambaza umeme vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili kimkoa mkoani Simiyu katika kijiji cha Igwata kata ya Nyabubinza wilayani Maswa .
Naibu Waziri Byabato amesema, jumla ya vijiji 151 kwa mkoa mzima vitapatiwa huduma ya umeme ambapo Wilaya ya Maswa ni vijiji 13, Bariadi 35, Meatu 48 na Busega vijiji 4 pamoja na vijiji vyote amabavyo havijafikiwa na huduma ya umeme pia vitafikiwa vyote bila kubakiza hata kimoja.
Naibu Waziri Byabato amewataka wananchi kushirikiana na Serikali ili kutoa ardhi na maeneo yao ili miundombinu ya umeme ipite ili waweze kupata huduma ya umeme na kuboresha maisha yao na huduma za kijamii.
Naibu Waziri Byabato amesisitiza kuwa, bei ya umeme ni shilingi 27,000 kwa wateja wanaohitaji njia moja ya kusafirishia umeme (single phase) na 139,000 kwa wateja wanaohitaji njia tatu za kusafirishia umeme (Three phase). Amewasisitiza wananchi kuchangamkia fursa hiyo ya kuunganishiwa umeme ambayo ni kichocheo muhimu cha maendeleo.
Aidha, Mhe. Byabato amemuagiza Mkandarasi anaetekeleza Mradi wa REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili kuwasha umeme katika kijiji cha Igwata ndani ya mwezi mmoja kuanzia leo tarehe 08/07/2021.
Kwa upande wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)) Naibu Waziri wa Nishati, ameagiza kufunguliwa kwa madawati ya kutolea huduma ili kuwasaidia wananchi kutopata usumbufu wa kusafiri umbali mrefu kwa ajili ya kulipia huduma ya umeme.
Amewasisitiza wananchi kushirikiana na TANESCO ili kuwaongoza kupata wakandarasi wanaofunga umeme majumbani ili kukwepa kutapeliwa na vishoka. Naibu Waziri Byabato amewashauri wananchi ambao bado hawapo tayari kuweka mtandao wa nyaya katika nyumba zao kutumia kifaa cha UMETA (Umeme tayari) ambacho mwananchi atafungiwa kwa 27,000 tu.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Wakili Stephen Byabato akiongea na wananchi wa kijiji cha Igwata wakati wa uzinduzi wa Mradi wa REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza uliofanyika tarehe 08 Julai, 2021 katika viwanja vya shule ya msingi Igwatakatika kijiji cha igatwa Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Stephen Byabato, akiwashauri wananchi kutumia kifaa cha Umeme tayari (UMETA) katika nyumba zao kwa wananchi ambao watakuwa hawajakamilisha pesa za kuwawezesha kusuka mtandao wa nyaya (wiring) katika nyumba zao wakati wa uzinduzi wa Mradi wa REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili uliofanyika tarehe 08 Julai, 2021 katika kijiji cha Igwata kata ya Nyabubinza wilaya ya Maswa katika mkoa wa Simiyu.
Mhe. Naibu Waziri wa Nishati akikata utepe ili kuzindua jiwe la msingi la Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijni, Mzunguko wa Pili katika Mkoa wa Simiyu
Naibu Waziri Nishati akibonyeza king’ora ikiwa ni ishara ya kuzinduliwa rasmi Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili katika mkoa wa Simiyu
Naibu waziri wa Nishati, Mhe. Stephen Byabato akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Aswege Enock Kaminyoge ( Wa pili kutoka kushoto kwa Naibu Waziri Byabato) pamoja na watendaji wa TANESCO na REA baada ya kuzindua jiwe la msingi la mradi wa REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment