NDEJEMBI AFANIKISHA MRADI WA MAJI WA MILIONI 600 JIMBONI CHAMWINO | Tarimo Blog

Charles James, Michuzi TV

BAADA ya kilio cha muda mrefu cha wananchi wa Kata ya Dabalo Wilayani Chamwino, Dodoma cha uwepo wa changamoto ya uhaba wa maji hatimaye Mbunge wa Jimbo hilo la Chamwino na Naibu Waziri Utumishi, Deo Ndejembi amefanikisha kutatua kero hiyo.

Kwa muda mrefu wananchi wa Kata hiyo wamekua wakililia changamoto ya maji na moja ya ahadi za Ndejembi wakati akiomba kura kwenye kata hiyo aliahidi kumaliza kero hiyo na kuhakikisha maji yanatoka.

Katika jitihada za kumtua ndoo mama katika kata ya Dabalo tayari Naibu Waziri Ndejembi amefanikisha upatikanaji wa kiasi cha Milioni 600 kwa ajili ya mradi mkubwa wa maji ambapo kisima kikubwa chenye uwezo wa kutoa maji muda pamoja na kuwekwa kwa tanki lenye ujazo wa Lita Laki Moja na Nusu.

" Niliahidi wakati wa kampeni zangu kwamba nitamaliza changamoto ya maji hapa Dabalo, hivyo niwaambie ujenzi huu wa kuchimba kisima na uwekwaji wa bomba umeanza kwa ajili ya kupeleka maji katika kisima ambacho kitakua na uwezo wa kuhifadhi maji Lita Laki Moja na Nusu.

Nimepambana Serikali ya Rais Samia imetupatia Sh Milioni 600 kwa ajili ya mradi huu ambao kama ambavyo Rais Samia mwenyewe amekua akisema anataka kumtua Mama Ndoo basi azma yake inakwenda kukamilika hapa Dabalo," Amesema Ndejembi.

Akizungumza na vijana wa Bodaboda katika kata hiyo Naibu Waziri Ndejembi amewashauri kujiunga katika vikundi ili aweze kuwaletea mafunzo ya kibiashara na kuwaunganisha na mabenki kwa ajili ya kupatiwa mikopo lakini pia kunufaika na mikopo inayotolewa na Halmashauri.

" Sisi vijana huwa hatuchangamkii fursa, Halmashauri kuna asilimia nne ya vijana kati ya zile 10 ni nyie kujiunga kwenye vikundi ili mpatiwe hiyo mikopo, nawapongeza akina Mama wamekua wanufaika wakubwa sana na wanajua kukimbilia fursa," Amesema Ndejembi.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Chamwino, Deo Ndejembi akizungumza na wananchi wa kata yake ya Dabalo alipofanya ziara ya kukagua mradi wa maji unaotekelezwa kwenye kata hiyo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Mbunge wa Jimbo la Chamwino, Deo Ndejembi akishiriki kuchimba mtaro utakaopitisha bomba la maji katika Kata ya Dabalo Wilayani Chamwino.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi, Deo Ndejembi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chamwino akiambatana na wataalamu wa RUWASA na Viongozi wa Kata ya Dabalo wamekagua mradi wa Maji wa Sh Milioni 600 unaotekelezwa kwenye kata hiyo.

 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Mbunge wa Jimbo la Chamwino, Deo Ndejembi akizungumzia na vijana wa bodaboda wa Kata ya Dabalo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2