Njombe:Watoto watatu wakiwemo pacha wakamatwa kwa tuhuma za kuiba kuku | Tarimo Blog

Na Amiri Kilagalila,Njombe

Watoto wawili wakike na wakiume (mapacha) wenye umri wa miaka 9 na wakiume mmoja mwenye umri wa miaka 11 wametekelekezwa na baba yao mzazi katika nyumba wanayoishi.

Taarifa zinaeleza kuwa, baba wa watoto mapacha anayefahamika kwa jina la Edward Chaula amewatelekeza watoto hao kwa  kuondoka na kuikataza jamii kuto kutoa msaada wowote kwa watoto hao.

Aidha jamii ilibaini kuwa watoto hao wametelekezwa baada ya watoto hao kuonekana wakizagaa mitaani wakiiba kuku ili wafanye kitoweo na kuacha kuhudhuria shuleni ndipo balozi msaidizi katika mtaa wa mpechi kuwachukua na kuwafikisha ofisi ya mtendaji ili kupata kibali cha kuwapeleka wilayani Ludewa aliko mama wa watoto hao.

Chanzo cha kutelekezwa kwa watoto hao kinatajwa kuwa ni migogoro iliyopo kati ya wazazi wao ambapo baba anatajwa kuwa amekuwa akimtishia usalama mama yao ajulikanaye kwa jina la Andowise Mtega endapo atafika maeneo ambayo wanaishi watoto hao.

Tukio hili limebainishwa na mwenyekiti wa mtaa wa mpechi kata ya Mjimwema mjini Njombe Onesmo Kilasi wakati wa mahojiano yake na kituo cha radio cha Kings Fm baada ya kupata taarifa za tukio kutoka kwa rai wema.

 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2