PROF. KABUDI AWATAKA WATUMISHI KATIBA NA SHERIA KUSHIRIKI UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA WIZARA NA KUTATHMINI UTEKELEZAJI WAKE | Tarimo Blog

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza na Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakati wa kufungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo kilichofanyika mkoani Morogoro.


Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akiwa na Katibu Mkuu Prof. Sifuni Mchome na Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju wamesimama maalum kwa ajili ya kuimba wimbo wa mshikamano daima kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika mkoani Morogoro.

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akizungumza wakati wa kumkaribisha Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi kufungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi la wizara hiyo kilichofanyika mkoani Morogoro.

.

Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria walioshiriki kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo wakifuatilia kikao hicho kilichofunguliwa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi mkoani Morogoro.







Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi hayupo pichani alipofungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo mkoani Morogoro.


Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Sifuni Mchome na Naibu katibu kuu Bw. Amon Mpanju katka picha ya pamoja bada ya kumaliza kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika mkoani Morogoro tarehe 17 Julai, 2021


……………………………………………………………………..

Na mwandishi maalum, Morogoro.

Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi amewataka watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria kushiriki katika utekelezaji wa majukumu ya wizara na kutathmini mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu hayo kwa pamoja ii kuleta tija na ufanisi ndani ya Wizara.

Prof.Kabudi alikuwa akizungumza na watumishi hao alipokuwa akifungua Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo lililofanyika mkoani Morogoro.

“Ni vyema kila mtumishi akashiriki kikamilifu katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa pamoja kama timu na kutathmini mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya Wizara,” alisema.

Prof. Kabudi pia amewataka watumishi hao kuhakikisha wanasoma na kuielewa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020 -2025 na kupanga kuitekeleza, kufahamu vipaumbele vya serikali ya Awamu ya Sita na jinsi vinavyopaswa kutekelezwa, kujitambua, kutambua nafasi na majukumu yao ndani ya Wizara na kuwa na utendaji kazi wa pamoja kama timu.

Prof Kabudi pia ametaka kila mtumishi wa Wizara kushiriki katika utendaji kazi wa pamoja na kushiriki katika ujengaji wa taswira ya Wizara ili kuwa na taswira inayoendana na mabadiliko ya nchi inavyokwenda ikiwa ni pamoja na kuongeza kasi ya kutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara ili umma upate kufahamu.

Amewataka watumishi hao kuhakikisha wanazingatia na kufuata sheria, taratibu na kanuni za Serikali kuwa waadilifu katika mawasiliano na kuongeza na kuimarisha mawasiliano na mashauriano ya kazi ndani ya Wizara ili kumfanya kila mtumishi kuelewa mambo yanayotekelezwa.

Prof. Kabudi pia amewapongeza watumishi hao kwa kutembelea ili kujionea kwa pamoja utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya ujenzi wa Bwawa la kufua Umeme wa Mwalimu Julius Nyerere huko Rufiji mkoani Pwani na Ujenzi wa Reli ya Kisasa kutokea mkoani Morogoro – Kilosa hadi Dodoma na kuwasihi wawe mabalozi wazuri kuelezea yanayoendelea katika miradi hiyo na kuendelea kuiunga mkono Serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria walitembelea miradi ya ujenzi wa Bwawa la kufua Umeme wa Mwalimu Julius Nyerere huko Rufiji mkoani Pwani na walipokuwa njiani kurejea jijini Dodoma walitembelea Ujenzi wa Reli ya Kisasa unaoendelea kutokea Morogoro – Kilosa hadi Dodoma
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2