PURA kuzindua kanzidata wataalam Petroli na Gesi | Tarimo Blog

Mkuu wa Kitengo cha Ushirikishaji wa Wazawa na Ujumuishaji wa Wadau wa PURA  Charles Nyangi akizungumza na waandishi Habari kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo kwenye maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba)jijini Dar es Salaam.
Mjiolojia was Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Samwel Magambo akizungumza  na waandishi wa habari Katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) wakiwa katika picha ya pamoja katika Banda la Mamlaka hiyo katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.

*Mwamko wa Wazawa katika sekta hiyo wazidi kuongezeka

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
MAMLAKA ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) inatarajia kuzindua kanzidata ya wataalamu wa sekta hiyo Julai 15 mwaka huu.

Kuanza kwa Kanzidata hiyo itajumuisha wataalam, wauzaji na watoa huduma katika tasnia ya petroli na gesi ili kuwezesha wawekezaji wa ndani na wa nje kuweza kupata wataalam sahihi na washirika wataofanya sekta hiyo kukua huku Pura ikiwa na jukumu la kudhibiti na kusimamia shughuli za mkondo wa juu katika utafutaji, uendelezaji na uzalishashaji wa mafuta na gesi Tanzania Bara na kutoa huduma za ushauri kwa Serikali kupitia Waziri anayehusika na maswala ya mafuta.

Akizungumza na Katika Maonesho ya ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha Ushirikishaji wa Wazawa na Ujumuishaji wa Wadau wa PURA Charles Nyangi amesema kulingana na kanuni na sheria za eneo hilo, Pura imeamriwa kuanzisha kanzidata kwa wauzaji na watoa huduma kuwezesha wawekezaji kupata wataalam sahihi ikiwa ni pamoja na wahandisi wa mafuta ya petroli, wasambazaji, watoa huduma pamoja na washirika wa biashara za mafuta na Gesi.

"Kanzidata hiyo itakuwa na data zote zinazohitajika ni pamoja na wataalam katika sekta hiyo, tumeweka sifa zao za awali na kuweka taarifa sahihi kwa wawekezaji kupata wataalamu kwa urahisi wanapokuja nchini kuwekeza, katika Sekta hiyo na kuweza kukuza uchumi wa nchi ”amesema Nyangi.

Nyangi amebainisha kuwa mchakato huo ulifanyika kwa umakini ili kuhakikisha wanaweka watu sahihi wanaohusika na kazi hizo na kuleta matokeo chanya Rasilimali za mafuta na gesi.

Aidha amesema ushiriki wa wazawa katika miradi ya petroli na gesi umeimarika hasa katika suala la ajira huku akiwahamasisha watanzania kuchangamkia fursa katika upande wa biashara hiyo.

"Uhamasishaji wa ushiriki katika sekta ya mafuta ambayo Pura inasimamia sekta ya hiyo kupitia utafutaji Maendeleo kwenye Sekta hiyo."Amesema Nyangi

Ameongeza kuwa wanahamasisha wenyeji kushiriki katika sekta hiyo ambayo katika miaka iliyopita kazi nyingi zilifanywa na wageni kutokana na kutokuwepo mwamko katika masuala ya mafuta na gesi.

Akibainisha kuwa tangu kuanzishwa kwa Pura, ushiriki wa ndani katika tasnia umeongezeka kutoka idadi ndogo kutoka Tatu (3) hadi 56 na hamasa ya kujenga mwamko juu ya fursa zinazopatikana katika sekta ya juu ya wenyeji kushiriki katika hizo ikiwa ni pamoja na mradi wa LNG ambao umeanza tena mazungumzo ya HGA.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2