RC RUVUMA AFANYA ZIARA YA KIKAZI YA KUSHITUKIZA KUKAGUA MIRADI YA UJENZI NAMTUMBO. | Tarimo Blog

NA Yeremias Ngerangera..Namtumbo.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert  Ibuge  amefanya ziara ya kikazi ya  kushitukiza katika wilaya ya Namtumbo kukagua ujenzi  wa zahanati na shule za sekondari zinazokamilisha umaliziaji ujenzi wa maabara .

Ibuge alianza ziara ya kushitukiza katika shule ya sekondari  Luchili,Kimolo na Lukimwa  wilayani hapa na kukagua mradi wa umaliziaji ujenzji wa maabara ya shule hizo na kisha kukagua nyaraka ikiwemo Leja ,fomu ya mapokezi ya vifaa (issue voucher) pamoja na mihutasari ya vikao mbalimbali vya kuomba kununua vifaa vya ujenzi katika shule hizo.

Pamoja na hayo mkuu wa mkoa huyo alihoji ushirikishwaji wa  wananchi katika ujenzi na kubaini kuwepo kwa ushiriki hafifu wa wananchi katika shughuli za ujenzi wa miradi ya maendeleo na kuuagiza uongozi wa shule  na bodi za shule kuhakikisha kamati zinawashirikisha wananchi ,kuwepo kwa utunzaji wa kumbukumbu za ujenzi zilizowekwa kwenye mafaili pamoja na vitabu vya kupokea na kutoa vifaa vya ujenzi .

Mbunge wa jimbo la Namtumbo Vitta Rashid Kawawa alimwambia mkuu wa mkoa kuwa serikali imeleta fedha za miradi ili wananchi wanufaike na miradi yao kwa kufanya kazi kubwa katika miradi hiyo kwa hela kidogo na miradi yenye ubora kwa kuwa miradi hiyo ni ya kwao .

Kawawa alisema hayo katika ukaguzi wa boma zahanati ya Misufini ambapo serikali imetoa fedha milioni 50 kumalizia zahanati hiyo na kutafutwa fundi mwingine tofauti na mafundi wa hapo kijijini waliojitolea nguvu zao bila kulipwa fedha yoyote mpaka kumaliza boma hilo na zinapopatikana fedha mafundi hao wanaachwa alisema kawawa kuwa sio sahihi na nidhambi kwa mwenyezi mungu kwani mafundi hao wanaweza kukamilisha kila kitu katika jengo hilo kwa gharama nafuu na hela kubaki kwa ajili ya kuanza hata kujenga nyumba ya mganga.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Jumma Pandu alimwambia mkuu wa mkoa huyo kuwa changamoto zilizojitokeza katika ukaguzi wa miradi hiyo pamoja na maagizo yaliyotolewa na mkuu wa mkoa yatafanyiwa kazi na kurekebisha kasoro zilizojitokeza katika ziara hiyo alisema Pandu.

Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo imepokea fedha za ukamilishaji ujenzi wa maabara kwa shule za sekondari 7 kwa kila shule kupokea kiasi cha milioni 30 na kati ya shule hizo mkuu wa mkoa alikagua ujenzi wa maabara katika sekondari tatu Luchili,Kimolo Lukimwa na kujionea ushirikishwaji hafifu wa wananchi na kuagiza kuwepo kwa ushirikishwaji kwa wananchi ili kuimarisha uwazi kwa wananchi na kupunguza malalamiko yasiyo yalazima.



 


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2