RUCU YAKARIBISHA WADAU WA ELIMU KUTEMBELEA BANDA LAO MAONYESHO YA TCU | Tarimo Blog


Madam Baby Baraka Chumaakizungumza na baadhi ya wananchi walio tem,belea katika banda la RUCU katika maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Na Humphrey Shao, Michuzi Tv
WADAU na wanafunzi wanaotaraji kujiunga na elimu ya juu wametakiwa kutembelea Banda la Chuo Kikuu Cha Ruaha ndani ya maonyesho ya vyuo vikuu vinavyoendelea mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Michuzi Tv katika viwanja hivyo Madam Baby Baraka Chuma Amesema wanafunzi wakifika katika Banda hilo watakutana na fursa mbalimbali ikiwemo udahili wa moja kwa moja.

"Tunawaalika wanafunzi wote waje hapa kwani hapa tunafanya udahili wa moja kwa moja na kuwashauri wanafunzi juu ya masomo yao watakapokuwa chuoni na nini wafanye hili wapate michepuo sahizi." Amesema Madam Chuma.

Ametaja kuwa RUCU inatoa kozi mbalimbali kuanzia ngazi ya cheti mpaka shahada ya kwanza kwa fani mbalimbali.

Amesema kuwa wanafunzi wanaosoma RUCU wamekuwa Bora zaidi katika Maeneo mbalimbali ya kazi pindi wanapomaliza shule.

Ametolea mfano wa wanafunzi wa shahada ya Sheria na wale wanaosoma kozi ya Diploma ya Phamasia kutoka chuoni hapo.

Ametaja kuwa wanafunzi wa Sheria usoma kwa miaka minne Hali ambayo uwasaidia kufanya vizuri pindi wanapokwenda kwenye shule kuu ya Sheria.

Alitoa wito kwa wazazi na walimu kujiunga na Chuo Cha RUCU hili waweze kupata elimu Bora.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2