SERIKALI NA UNESCO WAZINDUA MRADI MPYA WA KISAYANSI UTAKAOSAIDIA NCHI KIMAENDELEO | Tarimo Blog

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe amesema kuwa mpaka sasa hakuna sera ya sayansi , teknolojia na ubunifu zaidi ya kuwa na sera ya sayansi ilitungwa mwaka 1996 ambayo ndio inatumika kwa sasa. 

Prof. Mdoe aliyasema hayo jana mjini Morogoro wakati akizindua mradi wa kuboresha mifumo ya sayansi, teknolojia na ubunifu kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknololojia pamoja na Tume ya Taifa ya UNESCO. 

Alisema kuwa kama nchi na kwa kutambua umuhimu wa sayansi, teknolojia na ubunifu kwa sasa mchakato wa kuandaa sera ya sayansi, teknolojia na ubunifu unaendelea na kwamba wizara iko tayari kushirikiana na wadau mbalimbali katika kukamilisha uandaaji wa sera hiyo. 

“Covid imetundisha tuwe tunajitegemea wenyewe kwa kuwekeza kwenye tafiti za kisayansi na kama nchi mradi huu utasaidia tuko wapi na tunaelekea wapi,” alisema Prof. Mdoe. 

Awali akitambulisha mradi huo Mkuu wa kitengo cha Sayansi asilia kutoka UNESCO Keven Robert alisema kuwa mradi huo utawezesha kusaidia nchi kuimarisha mifumo ya sayansi, teknolojia na utafiti.

Aidha mradi huo pia utasaidia kuimarisha taasisi za kisayansi kufanya tafiti na kuweka mazingira wezeshi ya kufanya tafiti za kisayansi ambazo zitasaidia katika kutatua changamoto za wananchi, kukabiliana na majanga yakiwemo magonjwa mbalimbali na pia kufikia malengo ya maendeleo endelevu.

Robert alisema kuwa mradi huo utakuwa na maeneo10 ya utekelezaji ambapo baadhi ya maeneo ni pamoja na kuangalia uwekezaji katika tafiti za kisayansi ambapo matokeo ya tafiti hizo zinapouzwa zinaweza kuimarisha uchumi ya nchi.

“Mfano katika kipindi hiki cha janga la Corona yapo mataifa yaliyofanya tafiti za kisayansi na kutengeneza chanjo hivyo zinapouzwa mataifa hayo yamekuwa yakipata fedha na kukua kiuchumi,” alisema Robert.

Alitaja maeneo mengine yatakayoangaliwa katika mradi huo kuwa ni kwa namna gani tafiti za kisanyansi zinasaidia wananchi na kwa namna gani wananchi wanashirikishwa kwenye tafiti kwa kuzingatia usawa wa kijinsia. 

Kwa upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi mkazi wa UNESCO Faith Shayo alisema kuwa mradi huo utakuwa wa awamu mbili na matarajio ya mradi huo ni kuona nchi inazingatia maazimio 10 ambayo yaliazimiwa mwaka 2017 baada ya maazimo ya awali ya mwaka 1974 kufanyiwa maboresho.
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,  Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa uimarishaji wa mifumo ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu (STI) kwa ajili ya Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini Tanzania kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) na kutekelezwa kwa ushirikiano  wa UNESCO, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ya Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM) uliofanyika katika hoteli ya Flomi mjini Morogoro.
Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi.Faith Shayo akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO nchini wakati wa uzinduzi wa mradi wa uimarishaji wa mifumo ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu (STI) kwa ajili ya Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini Tanzania kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano na UNESCO, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ya Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM) uliofanyika katika hoteli ya Flomi mjini Morogoro.
Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-UNESCO) Bw. Joel Samwel akitoa salamu za NATCOM wakati wa uzinduzi wa mradi wa uimarishaji wa mifumo ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu(STI) kwa ajili ya Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini Tanzania kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano na UNESCO, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ya Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM) uliofanyika katika hoteli ya Flomi mjini Morogoro.
Mkuu wa kitengo cha Sayansi Asilia wa UNESCO, Bw. Keven Robert akitoa muhtasari wa mradi wa uimarishaji wa mifumo ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu(STI) kwa ajili ya Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini Tanzania kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano na UNESCO, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ya Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM) uliofanyika katika hoteli ya Flomi mjini Morogoro.
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe (wa tatu kulia) akikata utepe kama ishara ya kuzindua mradi wa uimarishaji wa mifumo ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu(STI) kwa ajili ya Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini Tanzania kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano na UNESCO, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ya Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM) uliofanyika katika hoteli ya Flomi mjini Morogoro. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa kitengo cha Sayansi Asilia wa UNESCO, Bw. Keven Robert (kushoto), Mkuu wa kitengo cha Elimu wa UNESCO nchini, Bi.Faith Shayo (wa pili kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-UNESCO) Bw. Joel Samwel (kulia).
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe (wa tatu kulia) akimkabidhi nakala ya mradi huo Afisa TEHAMA wa TAMWA Bw. Godwin Assenga mara baada ya kuzinduliwa katika hafla iliyofanyika hoteli ya Flomi mjini Morogoro. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa kitengo cha Sayansi Asilia wa UNESCO, Bw. Keven Robert (kushoto), Mkuu wa kitengo cha Elimu wa UNESCO nchini, Bi.Faith Shayo (wa pili kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-UNESCO) Bw. Joel Samwel (kulia).
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe (wa tatu kulia) akimkabidhi nakala ya mradi huo Afisa Mtafiti kutoka idara ya DRCP (COSTECH) mara baada ya kuzinduliwa katika hafla iliyofanyika hoteli ya Flomi mjini Morogoro. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa kitengo cha Sayansi Asilia wa UNESCO, Bw. Keven Robert (kushoto), Mkuu wa kitengo cha Elimu wa UNESCO nchini, Bi.Faith Shayo (wa pili kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-UNESCO) Bw. Joel Samwel (kulia).
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Taaluma, Utafiti na Ubunifu wa  (NM-AIST) Arusha, Prof. Anthony Mshandete akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa uimarishaji wa mifumo ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu(STI) kwa ajili ya Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini Tanzania kwa ufadhili wa Shirika la UNESCO, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ya Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM) uliofanyika katika hoteli ya Flomi mjini Morogoro.
Baadhi ya washiriki kutoka taasisi mbalimbali za sekta binafsi, serikali pamoja na jamii walioshiriki uzinduzi wa mradi wa uimarishaji wa mifumo ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu(STI) kwa ajili ya Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini Tanzania unaoratibiwa na UNESCO  kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ya Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM) uliofanyika katika hoteli ya Flomi mjini Morogoro.
Baadhi ya vikundi kazi vilivyowashirikisha taasisi za elimu, watunga sheria, watafiti, wizara, sekta binafsi, asasi za kiraia,jamii na vijana wakijadili changamoto mbalimbali katika sekta ya Sayansi Teknolojia na ubunifu wakati wa uzinduzi wa mradi wa uimarishaji wa mifumo ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu(STI) kwa ajili ya Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini Tanzania kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano na UNESCO, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ya Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM) uliofanyika katika hoteli ya Flomi mjini Morogoro.
Picha ya Pamoja
 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2