Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
FAINALI ya kumpata Mlimbwende wa wilaya ya lala Jijini Dar es salaam (Miss Ilala) inafikia tamati leo jumamosi katika ukumbi wa lamada hotel, huku Mashabiki na wadau wa tasnia ya Urembo wakikumbushwa kuvaa barakoa ukumbini.
Akizungumza na Michuzi Tv Muandaaji wa Shindano Hilo Lucas Rutainiwa amesema Shindano Hilo linatarajia Kufika tamati usiku wa lep Julai 31,2021 na mpaka Sasa Warembo wapo 17 kutokana na kuwepo kwa ugonjwa wa uviko 19 warembo hawakuweza kukaa kambini.
"Wote tunaelewa kuwepo kwa ugonjwa wa uviko 19 hivyo kwa Mwaka huu imekua tofauti na warembo wetu hawakukaa kambini Bali walikua wakihudhuria Mazoezi katika ukumbi wa lamada uliopo ilala jijini Dar es salaam na mchuano ni Mkali warembo wote ni wazuri na wenye akili timamu hivyo tunategemea tutapata Mwakilishi mzuri na atakawakilisha Mashindano ya Miss Tanzania"
Hata hivyo Rutainiwa amesisitiza usalama kwa Wadau na Mashabiki watakaohudhuria Hafla hiyo itakayofanyika katika ukumbi wa lamada uliopo ilala jijini Dar es salaam kuwahi mapema na kuvaa barakoa kwa usalama wa afya zao huku vitakasa vya mikono vitakuwepo Mlangoni.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment