Ujenzi wa Daraja katika Mto Mayugu katika eneo la Kabunde linalojengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe , Mkoani Katavi kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) litakalogharimu zaidi ya shilingi milioni 112 kwa kutumia fedha za mfuko wa barabara katika bajeti ya fedha ya mwaka 2020/2021
lengo la kufungua daraja hilo ni kunusuru adha ya wananchi kuvuka kwenye maji katika eneo hili wakati wa mvua . Pia kutoa huduma za usafiri na usafirishaji wa mazao ya wakulima kutoka shambani kwenda sokon.
Daraja hilo likikamilika linategemewa kutoa huduma kwa wananchi zaidi ya watu 91,313 na kuwahudumia wakulima zaidi 12,692 kwa ajili ya kusafirisha mazao kwenda maeneo mbalimbali kujipatia riziki.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment