Mwalimu wa VETA Singida Ladislaus William akiwa baadhi ya vyakula ambavyo vinaweza kuchanganywa pamoja na kupata Chakula cha lishe kwa ajili ya kuku.
Mashine ya kuchanganya chakula.
Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA) wabuni mashine ya kuchanganya Chakula cha Mifugo ikiwemo kuku kutokana na kuwepo kwa wafugaji wengi ambao wanatakiwa kuchanganya vyakula kwa uwiano.
Mashine hiyo imetengenezwa kwa ushirikiano kwa Vyuo viwili vya VETA ambavyo ni Singida pamoja na Songea.
Akizungumza katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar Salaam.Mwalimu VETA Singida, Ladslaus William amesema kufanya ubunifu kumetokana na kuwepo kwa changamoto kwa wafugaji wa kuku kuchanganya chakula.
Amesema wakati kubuni mashine hiyo imekuja kutatua changamoto hiyo na kwa sasa wafugaji wanaweza kuwa na mashine hiyo.
William amesema kuwa kujua mashine inafanya kazi walichukua mchanga ambapo ulichanganywa na kujua kaizi yake.
Amesema kupitia maonesho hayo wananchi wafike banda la VETA kuona na mashine hiyo na wale wafugaji wa kuku kupata mashine.
Aidha amesema kuwa kazi ya VETA kutoa sualuhu kwa jamii katika kurahisisha katika nynzo za kufanyia kazi hasa uchumi wa sasa unaokwenda na Teknolojia.
"VETA Kazi yetu ni kutatua changamoto kwa wananchi katika Sekta ya ufugaji kwenda kisasa kwa kuweza kupata kuku wenye ubora na kuingia katika soko bila kukutana na vikwazo vinavyotokana na lishe." Amesema William.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment