Na Linda Shebby,Bagamoyo
MWENYEKITI wa Baraza la Ushindani nchini 'Fair Competition Tribunal' (FCT) Jaji Stephen Murimi amesema kuwa asilimia ya kesi 90 zilizohusiana na masuala ya Ushindani wa kibiashara ziliamuliwa katika kipindi Cha 2019 na 2020.
Jaji Murimi alisema hayo alipozungumza na waandishi wa Habari katika semina elekezi ya simu tatu kwa Wajumbe wapya wa Baraza Hilo ambao wameteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
"Wajumbe hawa sita wapya wametoka katika fani mbalimbali ambapo tumepata wanasheria wanne,Mchumi mmoja na Profesa mmoja hivyo tumekutana hapa ili niweze kuwaelekeza yote wanayopaswa kuyafanya ndani ya Baraza letu"alisema Jaji Mrimi.
Akizungumza na Michuzi Blog Mjumbe mpya Dkt. Onesmo Kyauke Ali anamshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua hivyo ana ahidi kufanya kazi kwa ufanisi.
Dkt. Hanifa Massawe ambaye ni mwanamke pekee kwenye Baraza Hilo amesema atafanya kazi yake kwa uadilifu.
Mafunzo hayo ya siku tatu kwa Wajumbeyalifanyika Bagamoyo Mkoani Pwani.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment