Na Marco Maduhu, Shinyanga
Wananchi wa vijiji vya Uzogore na Bugwandege Kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga, wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, kwa kuwajengea daraja ambalo lina unganisha vijiji hivyo.
Wananchi wamebainisha hayo leo wakati Mbunge huyo ,alipofika kwenye daraja hilo kuangalia maendeleo ya ujenzi wake, ambalo lipo katika hatua nzuri ya ukamilishwaji.
Wamesema kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo kutawaondolea hofu ya kusombwa na maji kipindi cha mvua, ambapo maji yalikuwa yakijaa na kupita hivyo hivyo, huku baadhi ya wanafunzi wakikatisha masomo kwa muda.
"Tuna mshukuru Mbunge wetu Katambi kwa kutujengea daraja hili ambalo lina unganisha vijiji viwili vya Uzogore na Bugwandege, ambalo ni kiungo muhimu sana katika Shughuli za kiuchumi," amesema Emmanuel Martini.
"Pia daraja hili limetuondolea changamoto ya watoto kutokatisha vipindi tena vya masomo wakati wa mvua, kwa kuhofia kusombwa na maji," ameongeza.
Naye Diwani wa Ibadakuli Msabila Malale, amesema daraja hilo ni kiungo muhimu sana kwa maendeleo ya wananchi wa vijiji hivyo viwili, na kumpongeza Mbunge Katambi kwa kusikiliza kilio hicho cha wananchi.
Kwa upande wake Mbunge Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi, Vijana, na Ajira, Patrobas Katambi, amesema alipofanya ziara kwenye vijiji hivyo, alijionea mwenywe ubovu wa daraja hilo na kuamua kutafuta fedha za kulijenga.
Aidha amesema fedha za ujenzi wa daraja zilipatikana Sh.milioni 420 na sasa linaendelea kujengwa, na zimeshapatika fedha zingine kiasi cha Sh. milioni 90 kwa ajili ya ujenzi wa kingo.
Pia amewahidi wananchi hao wa Ibadakuli kuendelea kutatua changamoto zao ,ikiwamo ujenzi wa miundombinu ya Barabara, Afya, Elimu, Maji, na Umeme.
Katika hatua nyingine amewataka Watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassani, kwa kazi nzuri ambayo anaifanya ya kuwaletea maendeleo, na kuwapuuza wale ambao wanapinga kila kitu.
Muonekano ujenzi wa daraja ambalo linaunganisha vijiji viwili ya Uzogore na Bugwandege.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Ptrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, na Ajira, akikagua ujenzi wa daraja la Uzogore na Bugwandege ambalo lina unganisha vijiji hivyo, lililopo Kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akizungumza na wananchi wa Ibadakuli kwenye mkutano wa hadhara.
Diwani wa Ibadakuli Masabila Malale, akizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara.Diwani wa Vitimaalum Zuhura Waziri, akizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara.
Wananchi wa Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge Katambi.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment