Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Wakala wa Biashara na Leseni (BRELA) Roida Andusamile akimkabidhi cheti cha jina la Biashara Ibrahimu Kahamba alichopata ndani ya Maonesho ya Sabasaba.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
WAKALA Wakala wa Biashara na Leseni (BRELA) imesema kuwa wananchi wamekuwa na mwamko wa wa usajili wa majina ya Biashara na usajili wa makampuni.
Hayo ameyasema Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa BRELA Roida Andusamile wakati akitoa huduma kwa Wateja wanaotembelea Banda la BRELA katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam. Andusamile amesema katika maonesho hayo wanasajili majina ya Biashara, makampuni, alama za biashara na huduma, wanatoa leseni za biashara kundi A, leseni za viwanda na utoaji wa hataza.
Amesema kuwa wananchi watembelee Banda la BRELA kusajili na kupata taarifa mbalimbali zitazowasaidia katika usajili wa Majina ya Biashara na huduma nyingine kwani kwani wanapopata usajili kutoka BRELA wanazipa utu wa kisheria biashara zao.
"Tumedhamiria kuwafikia wananchi wetu katika kutoa huduma pale walipo na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wakati wa kusajili kwa njia ya mtandao kwani kwa sasa huduma zote zinatolewa kwa njia ya mtandao. "Amesema Andusamile.
Aidha amewahimiza wananchi kutembelee banda la BRELA katika maonesho ya Sabasaba kwani hawatajutia kufika hapo kutokana jinsi walivyojipanga.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment