WAZIRI NDAKI AWATAKA WATENDAJI SEKTA YA UVUVI KUTILIA MKAZO SHERIA YA UCHAKATAJI MABONDO | Tarimo Blog


Charles James, Michuzi TV

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amewataka watendaji wa sekta ya uvuvi wa wizara hiyo kutilia mkazo sheria ya uchakataji wa mabondo ambayo yamekua yakionekana kuchakatwa na wananchi wa maeneo mbalimbali badala ya viwandani kama sheria inavyoelekezwa.

Waziri Mashimba pia amewataka watendaji hao kudhibiti mfumo huo wa kuuza samaki mzima kabla ya kumchakata kwa sababu mfumo huo unakosesha Serikali mapato mengi ambayo yangepatikana kutokana na mauzo yanayotokana na Samaki huyo.

Aidha amewataka watendaji wakuu na wakuu wa idara za wizara hiyo kudumisha ushirikiano baina yao na watumishi waliopo chini yao ili kuchochea ufanisi kazini.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki wakati akizungumza na watendaji wa wizara hiyo pamoja na wakuu wa idara mbalimbali ambapo amewataka kutengeneza mazingira rafiki ya utendaji kazi kwa watumishi waliopo chini yao.

Amewataka watendaji wa wizara hiyo kufanya kazi kwa weledi bila kuogopa huku akiwahakikishia kuwa yeye yupo pamoja na wao na kwamba hana upande wowote wa watumishi.

" Niwahakikishie mimi kama Waziri wenu sina upande wa mtu yeyote nachohitaji kwenu ni ushirikiano kati yenu na watumishi waliopo chini yenu, ondoeni hofu fanyeni kazi kwa kuzingatia kanuni na taratibu za kazi.

Kwenu watendaji na wakuu wa idara msiwalinganishe watumishi wenu, kila mmoja ana kipawa chake, hawawezi wote kuwa sawa hata kama wako Idara Moja," Amesema Ndaki.

Waziri Ndaki pia amewataka watendaji wa juu kuzingatia matumizi mazuri ya lugha pindi wanapokua wanawakosoa walioko chini yao na siyo kutumia  lugha zenye kuudhi na zisizozingatia maadili yetu.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki akizungumza na Watendaji na Wakuu wa Idara wa Wizara hiyo leo jijini Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Abdallah Ulega.
Watendaji na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakimsikiliza Waziri wa Wizara hiyo, Mashimba Ndaki (hayupo pichani) wakati wa kikao cha pamoja kilichofanyika Wizarani Mtumba jijini Dodoma leo.

 Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof Elisante Ole Gabriel akizungumza kwenye kikao Cha  pamoja kati ya Waziri wa Wizara hiyo, Mashimba Ndaki na Watendaji na Wakuu wa Idara Wizarani hapo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2