Agricom Africa yaingia Makubaliano na Benki ya Kilimo TADB | Tarimo Blog

*Wakulima kuanza kutumia Trekta na Zana za kisasa za Kilimo kwa gharama nafuu

*Wanawake na vijana ni neema katika Sekta ya kilimo.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) imeingia makubaliano na Agricom kwa ajili ya ya kuwapatia wakulima nchini uwezo wa kujipatia matrekta na zana za   kisasa za Kilimo kwa gharama nafuu ambayo inatokana na mkopo kutoka katika benki hiyo.

Mkopo huo kwa wakulima utakuwa na riba  Kati ya asilimia na Nane (8) hadi 10 ambapo ndio Benki ya kwanza yenye lengo ya kwenda kutoa huduma kwa wakulima

Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo Mwenyekiti wa Agricom Afrika na Mwenyeki wa Sekt Binafsi Nchini (TPSF) Angelina Ngalula amesema makubaliano hayo ni kuwatoa wakulima katika Kilimo cha kujikimu na kwenda katika Kilimo cha biashara.

Amesema kuwa Agricom inataka kwenda na Kauli ya Rais Mama Samia Hassan Suluhu  ya kutaka kuwainua wakulima kwenda katika kilimo cha kisasa na kuleta matokeo ya kiuchumi kwa mtu mmoja moja na hatimaye kwa Taifa.

Ngalula amesema  Agricom ipo kwa ajili ya kutoa suluhisho kwa wakulima katika kuhakikisha wanapata mashine za kisasa na kuweza kuzalisha mazao mengi.

Aidha Mwenyekiti huyo amesema katika hatua nyingine wakulima wakikopa mashine hizo wataanzisha Mfumo wa ununuzi wa Mazao kwa kutafuta masoko wenyewe ili mkulima aachane na kuhangaika na mazao yao.

Amesema mashine na matrekta yapo katika mikoa mbalimbali huku matrekta 200 yakiwa yameshashuka bandalini kwenda kwa wakulima.

Nae Mkurugenzi wa Fedha wa TADB Derick Lugemala amesema ushirikiano huo na  Agricom ni wa mkakati unaolenga kuongeza idadi ya wakulima wanaotumia zana za kisasa na zenye gharama ndogo sana ikilinganishwa na riba za benki za biashara katika soko la sasa.

"Ushirikiano wetu na Agricom unawapatia wakulima wetu fursa mbili za kipekee zinazowafanya kupata uhaueni kwenye kununua zana za kilimo.ya kwanza ni kupunguzwa kwa riba kutoka asilimia moja (1)hadi  Nne (4)ya pili ni kupata ruzuku ya hadi asilimia Tatu(3) katika gharama halisi ya kila inaponununuliwa... Pamoja na tuna riba maalum kwa ajili ya wanawake na vijana ambapo mkulima anayeangukia katika makundi hayo atalipia riba ya asilimia 9tu .Hii ni ahaueni mkubwa sana kwa wakulima wetu,kwa sababu katika soko la kawaida la kibiashara ,riba zinaweza kupanda hadi asilimia 18.

Amesema kuwa TADB itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha mkulima ananufaika kwa Kilimo kwa kuachana na jembe la Mkono.

Mwenyekiti wa Agricom Afrika Angelina na Ngalula na Mkurugenzi wa Fedha wa TADB Derick Lugemala wakisaini makubaliano ya kuwapatia matrekta na zana za kisasa za Kilimo kwa gharama nafuu kutokana na mkopo kutoka benki ya TADB hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Agricom Afrika Angelina na Ngalula na Mkurugenzi wa Fedha wa TADB Derick Lugemala wakibadilishana Hati za  makubaliano ya kuwapatia matrekta na zana za kisasa za Kilimo kwa gharama nafuu kutokana na mkopo kutoka benki ya TADB hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.



Picha mbalimbali Mara baada  ya kusaini makubaliano Kati ya Agricom Africa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB).
 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2