AWAMU HII TUNAPELEKA UMEME VITONGOJINI BUMBULI - MAKAMBA | Tarimo Blog

 Raisa Said.


 Mbunge  Jimbo la Bumbuli Mkoani Tanga January Makamba amesema kuwa atahakikisha vijiji na vitongoji vya halmashauri hiyo ambavyo havijafikiwa na umeme vinafikiwa  ili viweze kuondokana na changamoto ya giza

Akizungumza katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo Makamba alisema wakati anaingia madarakani alikuta ni kata nne tu ndo zilikuwa  na huduma ya umeme lakini hivi Sasa kata 15 Kati ya 18 tayari zimeshafikiwa na huduma hiyo.

Alitaja kata tatu ambazo hazina umeme kabisa kuwa ni Milingano ,Kwemkomole na Kisiwani.

Mbunge huyo alisema kuwa alipoingia madarakani aliahidi kupeleka umeme kila Kijiji  na ahadi hiyo ameitimiza kwa kiasi kikubwa na Sasa anapigania kata zilizobaki  zinapate ili awamu nyingine aanze na vitongoji vyote katika Jimbo la bumbuli.

" Kama umeme huu ungekuwa haujafika kabisa arafu  Mbunge akaahidi kupeleka kwenye vitongoji basi  ujue huyo ni tapeli naomba muendelee kusubiri umeme utafika kwani maendeleo yakipatikana ata Mimi mbunge nafurahi"Alisema Makamba.

Makamba alisisitiza  kuwa ilani ya chama cha mapinduzi CCM inaelekeza kuwa
maeneo yote ambayo hayajafikiwa na umeme yafikiwe ili  wananchi wa maeneo husika waweze kuondokana na  giza na wakae kwenye mwanga.

Alisema kuwa  dalili  yakwamba  umeme utafika maeneo yote  tayari
baadhi ya nguzo zinaoneka  tofauti na miaka ya nyuma  iliyopita  hakukuwa na
nguzo hata moja hivyo endeleeni  kuwa na uvumili ili tuweze kumalizia  changamoto zilizopo na ahadi zake.

Mbali na umeme Makamba aliahidi  uboreshaji wa miundombinu mingine ikiwemo uboreshaji wa shule za msingi na sekondari  katika awamu hii  
lengo likiwa  ni kuweka mazingira bora  ya kujifunzia wanafunzi ili kuwapa hamasa ya kuongeza ufaulu katika masomo yao.

Alisema kwenye elimu kunachangamoto kubwa sana  na kila shule inaupungufu furani wa kitu na hili ni tatizo la nchi nzima na changamoto hiyo inapelekea ufaulu duni.

Wananchi wa Jimbo hilo wamempongeza Mbunge huyo kwa Kuendelea kuwasaidia katika suala zima la maendeleo hivyo wanaamini Mbunge wao kwa kushirikina na serikali umeme utafika kila mahali na ahadi alizoahidi  za kumaliza changamoto zinakamilika.

Mbunge wa jimbo la Bumbuli Mhe. January Makamba akiwa amembeba mmoja wa watoto wakati wa ziara yake jimbo humo kukagua maendeleo ya Miradi mbalimbali sambamba na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2