Na Zainab Nyamka, Michuzi TV
MAMLAKA ya majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wameanza utekelezaji wa mradi mkubwa wa usambazaji huduma ya maji safi kwa maeneo ya pembezoni mwa mji.
Mradi huo utakaotekelezwa ndani ya kipindi cha miezi 12 utahusisha maeneo ambayo hayakuwa na mtandao wa maji wa Dawasa.
Akiwa ameambatana na Mkandarasi pamoja na Mhandisi Mshauri, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii Dawasa, Neli Msuya amesema miradi hii inatekelezwa kwa ufadhili wa fedha kutoka Benki ya Dunia na unaendea kuondoa changamoto ya maji katika maeneo yasiyokuwa na mtandao.
Amesema, tayari wameshapata mkandarasi ambaye ni kampuni ya Ceytun/Kascco Joint Venture kutoka Uturuki na leo wamekuwa wanafanya kazi ya kumuonesha maeneo yanayotakiwa kupita mradi huo.
“Huu ni mradi mkubwa na unaenda kuondoa changamoto ya maji pembezoni mwa mji kwenye maeneo ambayo hayana mtandao wa maji wa Dawasa na tunatekeleza kwa ufadhili kutoka Benk ya Dunia,” amesema Msuya.
Amesema, mradi huu ni awamu ya kwanza na una thamani ya Bilioni 11.5 na baada ya kumaliza kwa ulazaji wa mtandao wa maji Dawasa itaendelea kusambaza kwa wananchi kwa kutumia fedha za ndani.
Ameongeza kuwa maeneo yatakayonufaika na mradi huo ni:
Kigamboni katika maeneo ya Feri, Tungi, Upendo na Vijibweni, Mtoni Kijichi katika mtaa wa
Butiama na Mwanamtoti, na eneo la Mbagala Mianzini, Dovya Chamazi, Bamia, Mbande na Kisewe.
Maeneo yote hayo ya mradi yatahudumiwa kwa kutumia mtambo wa Ruvu Juu, Ruvu Chini na Mtambo wa Mtoni.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment