MARUFUKU MIKUSANYIKO NA MAANDAMANO NDANI YA MKOA WA ARUSHA-RC ARUSHA | Tarimo Blog

 Na abel Paul Jeshi la Polisi Arusha
 
Leo tarehe 03.08.2021 Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalamaa Mkoa wa Arusha ambae pia ni Mkuu wa Mkuu wa Mkoa  wa Arusha JOHN MONGELLA alipokuwa akizindua chanjo kimkoa amepiga marufu mikusanyiko na maandamano ndani ya Mkoa wa Arusha.
 
Hayo ameyasema leo katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano AICC jijini Arusha ambapo amesema kuwa ustawi wa nchi na Mkoa wetu si maandamano "hivyo niwatake wananchi kutofuata Mkumbo wa wanasiasa ambao wanawashawishi kuandamana"

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa Mkoa wa Arusha ACP JUSTINE MASEJO leo Tarehe 03/08/2021 amepiga marufuku mikusanyiko na maandamano yeyote ndani ya Mkoa wa Arusha kwani atakeye fanya hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakao thubutu kuandamana.


 
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2