NA YEREMIAS NGERANGERA..NAMTUMBO
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Dkt Julius Keneth Ningu alipewa jina la Baba Namtumbo katika kijiji cha Mchomoro wakati wa mkutano wa hadhara wa wananchi wa kata ya mchomoro kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia majawabu.
AKiongea mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara mwananchi wa kijiji cha Mchomoro Adija Kapata alisema kwa namna mkuu wa wilaya huyo alivyosikiliza kero zao na kuzipatia majawabu wananchi wa kata ya mchomoro tunamwita Baba Namtumbo.
Dkt Ningu alifanya mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya mchomoro kusikiliza kero zilizowasilishwa kwake kutoka kijiji cha Songambele,Masuguru,Mchomoro na kilimasera kuhusu migogoro inayoendelea kati ya wafugaji na wakulima katika kata hiyo.
Katika mkutano huo Ningu alitoa nafasi kwa wananchi upande wa wakulima na wafugaji kutoa kero zao kwa kutoa ushahidi wa kuthibitisha kero wanazotoa na mara baada ya kusikiliza pande zote Dkt Ningu alitoa majawabu yakero zao.
Issa Kandimwa mkulima wa kijiji cha Masuguru alimthibitishia mkuu wa wilaya na kumwonesha majeraha ya mikuki aliyokuwa amepigwa na wafugaji wakati akipambana na wafugaji hao kulisha mifugo yao mazao yake na kutoa ushahidi wa kuripoti kituo cha polisi bila kupatiwa ushirikiano.
Saidi Hasani Kinombo kutoka kitongoji cha Mingwea kijiji cha mchomoro alimwambia mkuu wa wilaya ya Namtumbo kuwa wananchi ya kata ya Mchomoro hawapo tayari kuona maeneo yao ya kilimo yakiharibiwa na mifugo na wao kushindwa kuendesha shughuli za kilimo kama huko nyuma kwa sababu ya wafugaji.
Aidha Kinombo aliongeza kuwa kama sivyo ndivyo wananchi wa kata ya mchomoro wahamishwe na Serikali wapelekwe sehemu yoyote katika nchi hii ambayo wanaweza kuendesha shughuli zao za kilimo bila kugombana na wafugaji na kata ya mchomoro wabaki wafugaji hao.
Baada ya kauli hiyo mama wa kimang”ati Christina Nangai alionesha kutokwa na machozi na kumwomba mkuu wa wilaya kuwa sio wafugaji wote ni wakorofi bali wapo wachache na hata wakulima wengine nao ni wakorofi sio wote hivyo akamwomba kujenga mahusiano ili wafugaji hao wasiondolewe katika maeneo wanayokaa.
Hata hivyo Mkuu wa wilaya ya Namtumbo alisema migogoro katika wilaya ya Namtumbo kati ya wafugaji na wakulima inazidi kuongezeka kutokana na wafugaji kuthamini zaidi mifugo yao kuliko mazao ya wakulima na hilo linajitokeza kutokana na malalamiko mengi katika ofisi yake ni wafugaji kulisha mazao ya wakulima na kwa kuwa wilaya haikutenga eneo la kulisha mifugo hiyo hilo ndilo tatizo lililopo kwa sasa.
“Wafugaji ni Raia wa Tanzania na wanahaki ya kuishi popote katika nchi hii ilimradi hawavunji sheria wapokeeni wafugaji wanaotaka kuishi katika vijiji vyenu lakini hakuna maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kulisha mifugo yao katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo” alisema Dkt Ningu.
Kutokana na kuepuka migogoro inayotokea na inayotarajia kutokea kwa sasa kama hali hii ikiendelea wilaya ya Namtumbo kuanzia tarehe 11 mwezi septemba mwaka huu itaendesha zoezi la kuondoa mifugo iliyopo katika maeneo yasiyoruhusiwa.
Mkutano wa hadhara huo ulifanyika katika kiwanja cha ofisi ya kijiji cha Mchomoro ambapo wakulima na wafugaji katika kata ya mchomoro walipewa nafasi ya kuuliza maswali yao,kero zao ,maombi yao na baada ya kuhitimisha mkutano huo walimwita mkuu wa wilaya huyo Baba Namtumbo kwa namna alivyoweza kuwapa majawabu ya kero zao za muda mrefu.
DC Namtumbo 2.Afisa Ardhi na Maliasili Saimon Sambalu akitoa maelekezo ya migogoro ya mipaka.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment