Na Zainab Nyamka, Michuzi TV
Mwenyekiti wa Soka Mkoa wa Njombe Tobias Lingalangala amekabidhi kitita cha Shiling Milioni kumi (10,000,000) kwa uongozi wa timu ya Njombe kwa ajili ya usajili.
Timu hiyo iliyopo daraja la kwanza wamepatiwa fedha hizi ili ziwezw kuwasaidia katika suala zima la kusajili wachezaji watakaolera ushindani na kuisadia timu hiyo kurejea Ligi Kuu.
Akikabidhi fedha hizo kwa viongozi wa Njombe Mji, Lingalangala amewasihi kuwatafuta wachezaji wazuri na wenye uzoefu katika Ligi na kuwataka kuwa na umoja na mshikamo baina yao.
Mbali na hilo, Lingalangala ameonesha nia ya kuirejesha timu hiyo Ligi Kuu ikiwa ni pamoja na kuwajengea hostel (mabweni) ya kulala wachezaji ambayo yapo katika hatua za mwisho za umaliziaji.
Hatua hiyo imewafurahisha viongozi wa Njombe Mji na kuwashukuru kwa kazi kubwa anayoifanya kwa moyo ya kuhakikisha Njombe Mji inarejesha makali yake na kurejea Ligi kuu.
Aidha, wamemuhakikishia kuwa watazitumia vizuri fedha hizo katika usajili na hakutakuwabna mchezaji atakayedhulumiwa fedha zake za usajili.
Hostel zitakazokaliwa na wachezaji wa Njombe Mji zikiwa katika hatua ya mwisho ya umaliziaji kabla ya kukabidhiwa kwa Uongozi wa Timu hiyo
Mwenyekiti wa Soka Mkoa wa Njombe Tobias Lingalangala(wa pili kulia) akikabidhi kitifa cha fedha kiasi cha Milioni kumi (10,000,000) kwa Uongozi wa timu ya Njombe Mji ili kusaidia katika usajili kwa msimu wa 2021/22
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment