WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hajarizishwa na kasi ya ujenzi wa Hospitali ya Mkoa wa katavi, na kuiagiza Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kukabidhi usimamizi wa ujenzi huo kuwa chini ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Wizara kubaki mkaguzi wa mradi huo..
Amesema kuwa Shilingi Milioni 688 zilizotolewa na Serikali zikabidhiwe kwa Katibu Tawala Mkoa na aunde timu ya ujenzi na Mkuu wa Mkoa aijue ili kuwe na urahisi wa ufuatiliaji.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Agosti 27, 2021) alipokuwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo na utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi katika Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi, Amesema Serikali.
“Mikoa mingine yote tumefanikiwa Musoma tulikuwa na Hospitali kubwa ya kanda, Imekaa kwa miaka mingi, tulipowapa Mkoa walikamilisha haraka na sasa inafanya kazi, Hii Milioni 688 Malizieni itumike kukamilisha jengo la kwanza na lianze kutoa huduma.”
Aidha, Waziri Mkuu amesema kuwa Mheshimiwa Rais anataka kuona kila Mtanzania anapata huduma bora na za uhakika za afya pale alipo.
“Serikali inachokifanya sasa ni kuhakikisha tunajenga vituo vya Afya Kimkakati, palipo na zahanati 6 hadi 7 tunakuwa na kituo cha Afya ambacho kitatumika kama rufaa ana ya vituo vya Afya tunavyojenga sasa vinapima magonjwa yote, vinafanya upasuaji, vinamhudumia mama na motto lakini pia vina wodi za kulaza wagonjwa.”
Katika Hatua Nyingine Waziri Mkuu ametanabaisha kuwa tayari Rais ameridhia marekebisho katika tozo za miamala ya simu na hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Agosti Serikali itakuwa imetoa taarifa ya punguzo za Tozo hizo, huku akieleza namna ambavyo Serikali imetumia fedha ambazo tayari zimekusanywa kwa kupelekwa katika Miradi ya Maendeleo.
“Jumla ya fedha shilingi Bilioni 22.5 zimetolewa kwenye Halmashauri kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya 90 kwenye tarafa zisizo na vituo vya Afya, Ambapo kila kituo kimepatiwa fedha Shilingi Milioni 250 ya kuanza ujenzi.”
Kwa Upande wake Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Molel amemhakikishia Waziri Mkuu kuwa watatimiza maagizo yake ya kutaka Wizara ya fedha inakabidhi fedha za mradi huo kwa Katibu Tawala Mkoa wa Katavi na Wizara itaendelea kusimamia Mradi.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment