MWENGE WA UHURU WAENDELEA KUHAMASISHA UTUNZAJI WA MAZINGIRA KWA KUPANDA MITI KWENYE CHANZO MAJI CHA MTO KIZINGA | Tarimo Blog

 





Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Shabani Mkwanywe akitoa ufafanuzi kuhusu namna Mtambo unavyofanya kazi na usambazaji kupitia mchoro kwa Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi pamoja na Mkuu wa wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo mara baada ya Mwenge wa Uhuru kutembea kituo hicho cha kilichopo Manispaa ya Temeke Mkoani Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Shabani Mkwanywe(wa kwanza kulia) akimuongoza Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi eneo lililoandaliwa kwa ajili ya upandaji wa miti ya Mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2021 katika Chanzo cha maji cha Mto Kizinga Mtamb kilichopo Mtoni Manispaa ya Temeke leo.
Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi akipanda mti katika eneo la Uzalishaji maji wa Mtambo wa Mtoni ili kuendelea kutunza chanzo cha maji cha Mto Kizinga mara baada ya Mwenge wa Uhuru kutembelea kwenye kituo hicho kikongwa hapa mkoani Dar es Salaam.
Mkuu wa wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo akipanda mti katika eneo la Uzalishaji maji wa Mtambo wa Mtoni ili kuendelea kutunza chanzo cha maji cha Mto Kizinga mara baada ya Mwenge wa Uhuru kutembelea kwenye kituo hicho. Kulia ni Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Shabani Mkwanywe.
Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi pamoja na Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi wakisililiza taarifa fupi ya utunzaji wa Chanzo cha maji cha Mto Kizinga iliyokuwa ikisomwa na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Shabani Mkwanywe
Mkuu wa wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo akizungumza wakati wa Mwenge wa Uhuru ulipotembelea Chanzo cha maji cha Mto Kizinga kwa ajili ya kupanda miti ili kutunza chanzo cha Mto huo. Kulia ni Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi
Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi akitoa hotuba yake kwa wafanyakazi wa DAWASA, Manispaa ya Temeke pamoja na wananchi waliofika kwenye Chanzo cha maji cha Mto Kizinga kwa ajili ya kupanda miti ili kutunza chanzo hicho leo mara baada ya Mwenge wa Uhuru kuwasili eneo hilo leo. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo.
Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi pamoja na Mkuu wa wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo wakiwasili na Mwenge wa Uhuru kwenye Chanzo cha maji cha Mto Kizinga kwa ajili ya kupanda miti ili kutunza chanzo pamoja na kukagua Maendeleo ya chanzo hicho ambacho ni kikongwe hapa nchini.
Mwenge wa Uhuru ukiwasili katika Chanzo cha maji cha Mto Kizinga kwa ajili ya kupanda miti ili kutunza chanzo
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Shabani Mkwanywe akitoa ufafanuzi kuhusu Chanzo cha maji cha Mto Kizinga wakati wa kukagua chanzo hicho na Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi pamoja na Mkuu wa wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo mara baada ya Mwenge wa Uhuru kutembea kituo hicho cha kilichopo Manispaa ya Temeke Mkoani Dar es Salaam.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2