Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, anatarajia kuondoka nchini kesho tarehe 24 Agosti, 2021 kuelekea nchini Zambia kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema.
Sherehe za Uapisho wa Rais huyo Mteule wa 7 wa Zambia Mhe. Hichilema zitafanyika katika Uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium), Jijini Lusaka.
Katika msafara wake Mhe. Rais Samia ataongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM Ndugu Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Idara ya Oganaizesheni wa CCM Ndugu Maudline Cyrus Castico, Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe. Mizengo Peter Pinda, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mzee Kombo Hassan Juma, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mzee Henry Daffa Shekifu, na Mbunge wa Jimbo la Mtera na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mhe. Livingstone Joseph Lusinde.
Aidha, Rais mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete atashiriki katika sherehe hizo akiwa Kiongozi wa timu ya Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Jumuiya ya Madola.
Jaffar Haniu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment