RC SHIGELA AUNDA TUME KUCHUNGUZA CHANZO CHA MOTO ULIOTOKEA KITUO CHA UMEME MSAMVU MOROGORO | Tarimo Blog


NA Farida Saidy,Morogoro

MKUU wa Mkoa wa Morogoro Martin Shigela ametangaza kuunda tume kuchunguza chanzo cha moto uliozuka katika jengo la kuthibiti  mfumo wa upande wa  umeme msongo wa Kilovoti 33 la kituo cha kupozea na kusambaza umeme cha Msamvu Manispaa ya Morogoro na kusababisha Mkoa Morogoro kukosa huduma ya umeme kwa muda usio julikana.

Shegela ameyasema hayo mara baada ya kufika eneo la tukio na kujione madhala yaliojitokeza katika kituo hicho ambapo mpaka sasa chanzo cha moto huo hakijajulikana.

Aidha amesema kuungua kwa kituo huicho kumeleta madhala makubwa kwa shirika la umeme nchini,Viwandani,wafanyabishara na wananchi wa mkoa huo  kwa ujumla,ambapo serikali kwa kushirikiana na TANESCO itahakikisha huduma ya umeme inarejea kwa haraka.

Kwa upande wake Meneja wa TANESCO Mkoa wa Morogoro Mhandisi Fedgrace Shuma amewatoa hofu wakazi wa Mkoa wa Morogoro kuwa huduma ya umeme italeja ndani ya masaa 12.

Aidha amesema mitambo yote iliyomo ndani ya jengo lililoungua ipo salama isipo kuwa sehemu ya kuthibiti mfumo wa umeme ndio iliyoathilika zaidi na kusababisha kituo hicho kushindwa kufanya kazi muda.

Mhandisi Shuma ameongeza kuwa waatamu na mafundi wa Tansco wanaendela na kazi ya kuhakikisha huduma ya umeme inarejea kwa haraka iwezekanavyo.

Kwa upande wa Kamanda wa Jeshi Polisi Mkoa wa Morogoro Photnatuc  Musilm amesema jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulizi vikiwemo,jeshi la zima moto na uokoaji na jeshi la kikosi cha mzinga katika kuhakikisha hali ya usalama inahimalika katika eneo la tukio.

Akizungumza mara baada ya zoezi la uzimaji wa moto Mkaguzi wa jeshi la zima moto na uokoji mkoa wa Morogoro  Afande Neema Leonard  Msolwa amesema bado chanzo cha moto huo  hakijafahamika wanaendelea na uchunguzi wa chanzo hicho.


 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2