RC TABORA AWAOMBA WAFANYABIASHARA KUSAIDIA KUPANDISHA TIMU ZA MPIRA WA MIGUU ZA MKOA HUO | Tarimo Blog


NA TIGANYA VINCENT

MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani wadau wakiwemo Wafanyabiashara kusaidia timu za Mpira wa Miguu ili walau kuwepo zinazocheza Ligi.

Alisema Tabora inahistoria kubwa katika michezo na uzalishaji wa Vipaji wa Wachezaji ambao baadhi yao walifanikiwa kuchezea Timu ya Simba na Yanga

Balozi Dkt. Batilda alitoa kauli hiyo jana mjini hapa wakati wa uzinduzi wa Baraza la Biashara la Manispaa ya Tabora.

Alisema bado ya kuwa na Wachezaji kutoka Tabora waliofanya vizuri pia kulikuwepo na timu mbalimbali ambazo zilisaidia kuutangaza Mkoa.

Balozi Dkt. Batilda alisema imefika Wadau mbalimbali wakakakutana na kuangilia uwezekano wa kiziongezea nguvu timu zilizopo ili ziweze kupanda Daraja.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema Ofisi yake iko wazi katika kuweka mazingira wezeshi ambao yatawafanya Wachezaji kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali.

Alisema zitakapofanikiwa zitasaidia kukuza uchumiwa wa Mkoa wa Tabora kutokana na wageni ambao watakuja kuangalia Ligi.

Mkuu  wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani ( kushoto ) akibadilishana mawazo na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dkt. Isac Laizer (katika) mara baada ya kuzindua jana  Baraza la Biashara la Manispaa ya Tabora
 

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani (katikati) akitoa jana hotuba ya kuzindua Baraza la Biashara la Manispaa ya Tabora.

Mkuu wa Wilaya ya Tabora Dkt. Yahya Nawanda akifungua jana kikao cha uzinduzi wa Baraza la Biashara la Manispaa ya Tabora

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Biashara la Manispaa ya Tabora wakifuatilia hotuba ya uzinduzi wa Baraza la leo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2