Serikali Kuhifadhi Nyaraka za Utafiti wa Kiutamaduni Kidigitali | Tarimo Blog

Adeladius Makwega, WHUSM –Dodoma.
SERIKALI inaanza zoezi la kukusanya nyaraka zote za utafiti wa kiutamaduni na kuzihifadhi kigitali kwani imeonekana wazi nyaraka zote zilizohifadhiwa kwa mfumo wa zamani zinaweza kuhabika na kupotea kabisa kama zoezi hilo lisipofanyika kwa haraka.

Akizungumzia zoezi hilo Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Mnata Resani amesema kuwa mara baada ya Serikali kuhamia Dodoma mwaka 2017 baadhi ya nyaraka muhimu zilibaki Dar es Salaam na maeneo mengine kwa hiyo ili ziweze kutumika na kuweza kupatikana kwa urahisi ni lazima zihamishiwe katika kwenye mfumo wa kigitali.

“Zisipofanyiwa hivyo zinaharibika kwa haraka, zikiharibika siyo rahisi kupatikana tena, maktaba hai inayotoa simulizi hizo haipo tena kwani watu wa namna hiyo wengi wao wamefariki.” Aliongeza Dkt.Mnata.

Alibainisha kuwa mara zoezi hilo litakapo malizika basi kutapatikana takwimu sahihi za tafiti na kumbukumbu muhimu zitakazotumika kuhuisha Sera ya Utamaduni ya mwaka 1997 na rejea za wadau wa utamaduni.

Nyaraka hizo zitawekwa kwenye tovuti ya Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo (http://www. Habari.go.tz) na mitandao ya kijamii ili kila Serikali Kuhifadhi Nyaraka za Utafiti wa Kiutamaduni Kidigitali.
Afisa Utamaduni, Bi Hadija Kisubi.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2