SERIKALI YAAGIZA UTOAJI WA VIBALI VYA ELIMU MSINGI KUANGALIA UTEKELEZAJI WA AFUA ZA HALMASHAURI | Tarimo Blog







Na Asila Twaha - Dodoma

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mtaa anayeshughulikia elimu Gerald Mweli ameagiza utoaji wa vibali kwa miradi mipya inayoanzishwa na wadau wa sekta ya elimu kwa kuangalia utekelezaji wa afua zao katika halmashauri ambazo hazina wadau au zina wadau wachache.

Agizo  hilo amelitoa  jana  wakati wa kufunga warsha ya siku tatu, iliyokutanisha asasa 400 zinazotoa huduma katika  elimu msingi  nchini yenye kauli mbiu inayosema 'TUPANGE NA KUTEKELEZA KWA PAMOJA MIRADI YENYE TIJA KWA MAENDELEO YA ELIMU MSINGI.'

Ameendelea kufafanua kuwa  kumekuwa na mtawanyiko usio sawa wa wadau unaochangia ongezeko la tofauti ya ubora wa elimu kimkoa na halmashauri, hivyo amehimiza kuwepo kwa vikao vinavyokutanisha asasi na wadau wa elimu ili kuratibu ushirikiano kati ya Serikali na wadau na kutaka vikao vifanyike katika ngazi ya halmashauri na mikoa.

“ Nawaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Mikoa yote nchini kuhakikisha wanaanzidata za wadau wote wanaosaidia katika utoaji huduma katika elimumsingi katika halmashauri zenu na kuandaa  vikao vya wadau, angalau vikao vinne kwa ngazi ya halmashauri na viwili katika ngazi ya mikoa kila mwaka kwa lengo la kutathimini utekelezaji miradi kila mwaka” amesisitiza Mweli. 

Mweli amesema Mikoa ihakikishe inawasilisha taarifa ya utekelezaji wa maelekezo haya kila robo ya mwaka, kwa upande wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI kutakuwa na vikao mara mbili kila mwaka.

Aidha, ametumia fusra hiyo kutoa rai kwa asasi za kiraia zinashughulika sekta ya elimu kuendelea kuungana na Serikali katika kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2