Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga ,Mhe.Abdallah Ulega akizungumza leo na vijana wa Jogging kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo baada ya kumaliza kushiriki Jogging.Mhe Ulega amewaomba vijana wa wilaya hiyo kuchangamkia fursa ya mikopo inayotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga ambayo haina riba,amesema mikopo hiyo itawasaidia kujikwamua kiuchumi na kuongeza pato la Taifa.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega (katikati) leo ameshiriki mbio za pole pole Jogging na vijana wa maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Mkuranga, kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mohamed Mwela. (Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi TV)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega (kulia) na vijana Jogging kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, wakipasha moto misuli baada ya kumaliza kushiriki Jogging.Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Mkuranga,Mariam Ulega (kulia) na vijana Jogging kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, wakipasha moto misuli baada ya kumaliza kushiriki Jogging.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Mkuranga,Mariam Ulega akiwa miminia uji vijana Jogging kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi TV)
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment