VIJANA wa Heavenly Culture, World Peace, Restoration of Light (HWPL) 'Tamaduni ya Mbinguni, Amani Ulimwenguni na Kurejeshwa kwa Nuru' (HWPL) wameshiriki kupaka rangi katika shule ya msingi ya Kinondoni Julai 31, 2021 jijini Dar es Salaam.
Vijana hao wamepaka rangi katika shule hiyo ya Msingi wakiwa na lengo la kutangaza kazi ya amani hapa nchini.
Akizungumza mara baada ya kupanga rangi katika shule ya msingi kinondoni Mwanachama wa HWPL,Stephen Michael alisema kuwa vijana hao wanatangaza amani hapa nchini kwa kusaidia jamii na kwa shule ya msingi kinondoni wamesaidia kwa kupaka rangi.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Msingi Kinondoni, Saidi Kibode
Amewashukuru wana HWLP kwa kuisaidia shule hiyo kwa kupaka rangi katika kuta za madarasa za shule hiyo.
Licha ya hilo Mkuu wa shule aliwaomba wadau wengine wanaoweza kuaidia kama walivyofanya HWPL katika shule hiyo wasaidie kupaka rangi katika madarasa yaliyobakia.
Hata hivyo amewaomba waweze kufanya katika shule nyingine ambazo miundombinu ya madarasa rangi zake zikiwa nimeshachunika.
VIJANA wa Heavenly Culture, World Peace, Restoration of Light (HWPL) wakindaa rangi kwaajili ya kwenda kupaka katika kuta za shule ya msingi kinondoni jijini Dar es Salaama.
Vijana wa Heavenly Culture, World Peace, Restoration of Light (HWPL wakipaka rangi katika shule ya Msingi kinondoni.
Picha ya pamoja ya Vijana wa Heavenly Culture, World Peace, Restoration of Light (HWPL) mara baada ya kupaka rangi katika shule ya Msingi Kinondoni jijini Daar es Salaam.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment