WADAU WATOA MAONI MAREKEBISHO YA KANUNI ZA SHERIA YA EPOCA | Tarimo Blog

Naibu Katibu Mkuu wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi akifungua Mkutano wa wadau wa huduma za mawasiliano ili kutoa maoni kwenye rasimu ya maboresho ya kanuni 4 za Sheria ya Udhibiti wa Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta jijini Dodoma.

Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Philip Filikunjombe akizungumza kwenye Mkutano wa wadau wa huduma za mawasiliano ili kutoa maoni kwenye rasimu ya maboresho ya kanuni 4 za Sheria ya Udhibiti wa Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta jijini Dodoma



Baadhi ya wadau wa huduma za mawasiliano wakifuatilia mkutano uliowakutanisha wadau hao kwa ajili ya kutoa maoni kwenye rasimu ya maboresho ya kanuni 4 za Sheria ya Udhibiti wa Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta jijini Dodoma



Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania Deodatus Ballile akizungumza kwenye Mkutano wa wadau wa huduma za mawasiliano ili kutoa maoni kwenye rasimu ya maboresho ya kanuni 4 za Sheria ya Udhibiti wa Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta jijini Dodoma



Mwakilishi kutoka Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Umoja wa Haki za Kupata Taarifa (CORI) akizungumza kwenye Mkutano wa wadau wa huduma za mawasiliano ili kutoa maoni kwenye rasimu ya maboresho ya kanuni 4 za Sheria ya Udhibiti wa Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta jijini Dodoma



Mwakilishi kutoka Umoja wa Vyombo vya Habari vya Dini Tanzania Dkt.Vernon Fernandos akizungumza kwenye Mkutano wa wadau wa huduma za mawasiliano ili kutoa maoni kwenye rasimu ya maboresho ya kanuni 4 za Sheria ya Udhibiti wa Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta jijini Dodoma



Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) Samwel Nyalla akizungumza kwenye Mkutano wa wadau wa huduma za mawasiliano ili kutoa maoni kwenye rasimu ya maboresho ya kanuni 4 za Sheria ya Udhibiti wa Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta jijini Dodoma

…………………………………………………..

Na Faraja Mpina na Colnelia Munyi, DODOMA
Serikali imewakutanisha wadau wa Sekta ya Mawasiliano na Habari kujadili na kutoa maoni kwenye rasimu ya marekebisho ya kanuni nne za Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA). Kanuni hizo ni kanuni za leseni, kanuni za maudhui mtandaoni, kanuni za miundombinu ya utangazaji kidijitali na kanuni za maudhui ya redio na runinga

Akifungua kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi amesema kuwa Serikali imeona
umuhimu wa kuwaita wadau hao ili kupata maoni yao kwasababu wao ndio watekelezaji wa kanuni hizo.


Dkt. Yonazi amezungumza na wadau hao na kuwaeleza kuwa matamanio ya Serikali ni kuboresha mazingira ya watoa huduma za mawasiliano na habari nchini ili wananchi waweze kunufaika na kufaidi bidhaa na huduma bora za mawasiliano Ameongeza kuwa hadhira hiyo imekutana kwa ajili ya kufanya maboresho ya kanuni hizo kwa kutoa maoni yao katika maeneo ambayo yamefanyiwa mapitio hivyo ushirikiano wao na mchango wao unahitajika ili kufikia malengo yaliyokusudiwa

Naye Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.
Philip Filikunjombe amesema kuwa maboresho ambayo wadau wanatolea maoni yanaenda
kuleta mabadiliko katika Sekta ya Mawasiliano na Habari kwa kutenganisha kati ya watoa
huduma za maudhui mtandaoni kama chombo cha habari na wale wanaotoa maudhui
ambayo hayahusiani na vyombo vya habari

Amesema kuwa maboresho hayo yataenda kutatua sintofahamu ya nani anatakiwa kupatiwa leseni ya kuweka maudhui mtandaoni pamoja na kushusha ada ya leseni hizo kwa mwaka ambapo maombi ya leseni kwenye rasimu ya hiyo imeshuka kutoka shilingi laki moja hadi 50,000/= na ada ya leseni kwa mwaka imeshuka kutoka shilingi milioni moja hadi shilingi laki 5 kwa mwaka.


Aidha amezungumzia kanuni zilizopo kwa sasa zinawataka watoa huduma wa redio na
runinga kuomba leseni ya kutaka maudhui yaleyale kuonekana mtandaoni lakini rasimu hiyo ya maboresho ya kanuni hawatatakiwa kuomba leseni tena ili vipindi vyao kuonekana kupitia mtandao.

Dkt. Filikunjombe amezungumzia maboresho ya kanuni hizo kuwa yanaenda kupunguza
ada ya leseni ya kurusha matangazo ya redio na runinga kwa asilimia 30 na kuruhusu vituo vya redio na runinga kujiunga na vituo vingine kurusha maudhui yao bila kupata kibali kutoka TCRA isipokuwa watatakiwa kupeleka mpangilio wa vipindi unaoonesha kuwa atajiunga na kituo kingine.

Amesema kuwa maboresho hayo yanaenda kuhakikisha ving’amuzi vyote vinaonesha
chaneli za bure bila kujali ni king’amuzi cha kulipia au la ili kuongeza wigo wa wananchi
kupata taarifa.Maboresho mengine yaliyofanyika ni katika vipengele vya matangazo ya mubashara na
kuruhusu runinga za kulipia kuchukua matangazo na kubadili leseni ya redio na runinga za jamii kutoka leseni kubwa kwenda kuwekwa kwenye kundi la leseni ndogo.

Aidha, wadau mbalimbali walitoa maoni kuhusu rasimu ya kanuni hizo kwa makundi
wakiwemo wadau kutoka Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CORI), Baraza la Habari

Tanzania (MCT), MISA Tanzania, Umoja wa Makampuni ya Simu Tanzania (TAMNOA),
Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Wamiliki wa Ving’amuzi na Jukwaa la Wahariri
Tanzania.

Kanuni nne zilizofanyiwa maboresho ni miongoni mwa kanuni 22 za mawasiliano na
utangazaji zinazosimamiwa na TCRA ambapo kanuni 18 zipo chini ya Wizara ya
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na kanuni 4 zipo chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2