Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Usanganya Wilayani Sikonge wakipata mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliratibiwa na Mpango wa Kurasimisha Rasimali na Biashara ya Wanyonge Tanzania (MKURABITA)
NA TIGANYA VINCENT
WAKAZI wa Wilaya ya Sikonge ambao maeneo yao yamepimwa na kupata hati miliki za kimila wametakiwa kutumia mafunzo waliopatiwa kufanya shughuli za maendeleo ambazo zitawawezesha kubadilisha maisha yao
Kauli hiyo imetolewa jana katika Kijiji cha Usanganya kilichopo wilayani Sikonge na Meneja Urasimishaji wa Rasilimali na Ardhi Vijijini kutoka Ofisi ya Rais , Mpango wa Kurasimisha Rasimali na Biashara ya Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Antony Temu wakati akihitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo wa Wananchi waliorasimisha ardhi kutumia hati miliki za kimila.
Alisema mafunzo waliopata kuhusu umuhimu wa utunzaji wa kumbukumbuku za kilimo na biashara ili kujua mapato na matumizi kwa ajili ya kuwasaidia kuwa na mipango wakiyazingatia yatawaondoa katika umaskini na kuongeza vipato vyao.
Temu alisema ufugaji nyuki kwa kutumia miznga ya kisasa na elimu ya ufugaji kuku wa kienyeji ambao itawawezesha kuwa na chanzo cha ukakika cha mapato.
Aliongeza somo la kuongezea thamani ya ardhi kwa kupanda mimea ya kudumu ikiwemo mikorosho inawapa fursa ya kunufaika na kukopeshwa na Taasisi za Fedha.
Temu alisema uchumi wa wananchi wengi wa vijijini unategemea kilimo na hivyo somo la kilimo biashara litawasaidia kuondokana na uzalishaji wa kimazoea wa kulima ili kupata mazao ya kujikimu na kuingia katika uzalishaji unaolenga kupata ziada ambayo itawasaidia kujiapatia fedha kwa ajili ya maendeleo yao.
Alisema kuwa MKURABITA baada ya kutoa masomo hayo kwa kushirikiana na Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge watafuatilia kuona kama elimu waliyopata imewasaidia kubadilika kwenye maisha ya waliorasimishwa maeneo yao
Temu alisema imewasaidia Watu waliorasimishiwa ardhi kuwaunganisha na Taasisi za Kifedha ikwemo Benki ya CRDB na baadhi yao wamefungua akaunti ikiwa ni njia ya kueleka kutafuta mikopo kwa ajili ya kilimo biashara.
Alisema Benki ya CRDB kupitia Kitengo chake cha Kilimo biashara imewaonyesha kuwa wakulima wanayo fursa ya kupata mikopo ya kufanya kilimo biashara kama watakuwa wameendeleza maeneo yao kwa kupata miti ya mikorosho na kuondokana na kuwa mapori.
MKURABITA wakiwa Mkoani Tabora wamefanikiwa kutoa mafunzo katika Vijiji vitatu vya Mole, Usanganya na Kipanga wilayani Sikonge.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment