Waziri wa Kilimo aagiza Kaimu Meneja wa Kitengo cha Ununuzi wa Mbolea aondolewe kupisha uchunguzi | Tarimo Blog

Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda akizungumza na wadau wa Mbolea nchini kujadili changamoto zinazowakabili waagizaji wa mbolea. Mkutano huo umefanyika leo Agosti 9, 2020 Katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

WAZIRI wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda ameagiza kuondolewa kwa Kaimu Meneja wa Kitengo cha Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja (BPS) kilichopo katika Mamlaka ya Mbolea Tanzania (TFRA) Nganga Nkonya na kuhamishiwa Wizarani kwa ajili ya kupangiwa majukumu mengine.

Profesa Mkenda ametoa agizo hilo leo Agosti 9, 2021 jijini Dar Es salaam wakati wa mkutano wake na wdau wa Mbolea nchini unaolenga kujadili changamoto zinazowakabili waingizaji. wa mbolea nchini na njia bora ya kufanya mbolea Ishuke bei ili wakulima watumie mbolea, wazalishe kwa tija na waingizaji wa mbolea wanufaike na biashara ya mbolea

Waziri Mkenda amesema agizo la kuondolewa kwa Meneja huyo ni kutokana na hujuma ya kuchelewesha Watu kupata namba ya malipo (control number) kwa ajili ya kuagiza mbolea jambo ambalo watu wanaoagiza wamekuwa wakipata Changamoto wakati wakitaka Kuagiza Mbolea .

Profesa Mkenda Amesema kuwa amekuwa akipata malalamiko kutoka kwa wadau wa mbolea ambapo wamesema kuwa Meneja huyo amekuwa akiwazungusha kupata control number kwa ajili ya kuagiza mbolea kutoka nje ya nchi na pia kuweka namba ya simu ya mtu asiyejulikana na wakipiga wanaongea na mfugaji kutoka shinyanga.

Hata mimi imenishangaza namba ya simu iliyowekwa kwenye tangazo siyo simu yaTFRA na tangazo ni la mbolea.

Hata Hivyo amesema Amebaini Kuwa Namba Ya Simu Iliyowekwa Kwenye tangazo la uagizwaji wa mbolea sio ya Wizara bali ni ya mtu binafsi ambaye hausiki kabisa na masuala ya mbolea jambo ambalo anasema anashindwa kuelewa sababu za wao kufanya hivyo.

Katika hatua nyingine Waziri Profesa Mkenda amesema kuwa tayari wameshaondoa ule utaratibu wa uagiza mbolea kwa kutumia zabuni na badala yake wameweka utaratibu wa kila anayetaka kuagiza ikiwa ni njia ya Kushusa bei ya mbolea.

Mkenda amesema Kwa sasa Mbolea Katika Soko La Dunia Imepanda bei ila Kwa utaratibu wa kuagiza kwa kila mwenye uwezo utasaidia kuleta ushindani hivyo kupitia njia hiyo bei ya mbolea itashuka.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2