WAZIRI WA MAJI ARIDHISHWA MABORESHO YA MRADI WA MAJI GEITA | Tarimo Blog

 WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso ametembelea mradi wa maji Mharamba katika jimbo la Geita vijijini na kuridhishwa na maboresho yaliyofanyika na kupelekea vituo  vilivyokuwa havitoi maji kuanza kutoa huduma. 


Waziri Aweso ametoa maagizo kuwa vituo 3 vilivyobakia vianze kutoa huduma katika kipindi cha wiki mbili ikiwa ni pamoja na kufanya upanuzi wa mradi huu mkubwa pamoja na kuwaunganishia wananchi majumbani. Mradi huu una jumla ya vituo 20 na kwa sasa jumla ya vituo 17 vinatoa huduma kutoka katika tanki la lita 135,000.

Aidha Mh.Aweso amezitaka kamati za maji vijijini kuweka utaratibu mzuri wa matumizi na ukusanyaji wa fedha kutokana na uwepo wa baadhi ya kamati kuvuja fedha zinazokusanywa kwenye miradi.

Aweso ameyasema hayo wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi Wilayani #Geita kwenye kijiji cha Mwaramba,Kata ya #Nkome.
Kufatia uwepo wa taarifa kutokuwa sahihi ya kamati ya Maji kijiji cha Mwaramba kwenye suala la makusanyo.

Kufatia Hali hiyo Mkuu wa wilaya ya Geita, ambaye pia ni kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita, #Wilson Shimo ameliagiza Jeshi la Polisi na Takukuru kuwakamata na kufatilia uchunguzi wa mradi huo.





 
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2