Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), umehitimisha rasmi mchakato wake wa kusajili na kutoa Leseni za Biashara Papo kwa papo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Afrika Mashariki yaliyofanyika kwa siku tano jijini Dar es Salaam.
Maonesho yalifanyika kwenye viwanja vya ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini na wamefanikiwa kuwahudumia watu zaidi ya 200.
Akizungumza katika maonesho hayo Ofisa Leseni wa BRELA Robert Mashika amesema kuwa watu mbalimbali wametokeza kusajili majina ya Biashara na Makampuni na kupatiwa elimu.
"Katika siku hizi za maonesho haya tumekuwa na muda mzuri wa kutoa elimu na kujibu maswali mbalimbali ya wananchi na tumeweza kuwahudumia watu zaidi ya 200" amesema Mashika.
Mmoja wa wateja waliohudumiwa na kupatiwa Cheti chake papo kwa papo ni Dk. Hamisi Mahuna aliyekuwa na ndoto ya kuanzisha huduma za afya ambapo amesema kuwa ndoto zake zimetimia kwani yeye alifika ili ajue taratibu za kufuata lakini amejikuta amefanikiwa kufanya usajili na kupewa Leseni yake kwa muda mfupi.
"Nawashuru sana wafanyakazi wa BRELA wamenisaidia sana na kwakweli wanafanyakazi kwa ufanisi wa hali ya Juu sana leo hii nimefika hapa wameweza kuthibitisha jina langu la Biashara na kunisajili hapa hapa hili limenifurahisha sana" amesema Dk.Mahuna .
Ameongeza BRELA imekuwa ikifanyakazi kubwa hasa kwa kujikita kutoa Elimu kwa wananchi na hivyo kuwasihi watumishi wa taasisi hiyo kuendelea kufanyakazi bila kuchoka kwani wananchi wanaimani kubwa na Taasisi hiyo.
Hata hivyo kumalizika kwa maonesho hayo kunaipa fursa BRELA kujipanga tena kwenda kupiga kambi ya siku kumi Mjini Geita yatakapofanyika maonesho mengine makubwa ya Teknolojia ya Sekta ya Madini yanayotanariwa kuanza Septemba 16 hadi Septemba 26 Septemba mwaka huu.
Wakati timu nyingine ikipiga kambi jijini Mwanza kwenye maonesho ya 16 ya Biashara ya Afrika Mashariki yaliyoanza August 28 na kumalizika Septemba 5 mwaka huu.
Dkt. Hamis Mahuna (kulia) akizungumza na Maofisa wa BRELA Ofisa Usajili Ruth Mmbaga (wa kwanza kishoto aliyesimama), na Ofisa Tehama Hillary Mwenda (wa pili kushoto aliyekaa) alipokuwa akiwashukuru Maofisa hao mara baada ya kufanikiwa kusajili jina la Biashara na kupewa Leseni yake Papo kwa papo kwenye maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Afrika Mashariki yaliyomalizika leo jijini Dar es Salaam.
Ofisa Leseni wa BRELA Robert Mashika (kulia) na Ofisa Tehama Hillary Mwenda (kushoto) wakijadiliana jambo mara baada ya kufanikisha kumaliza zoezi la kusajili majina mbalimbali ya Biashara na kutoa leseni katika maonesho hayo
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment