DC MPOGOLO AKABIDHI PIKIPIKI KWA WATENDAJI 16 WA KATA WILAYANI SAME | Tarimo Blog


Charles James, Michuzi TV

WATENDAJI wa Kata 16 Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro wamepatiwa pikipiki ili kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato, usimamizi wa miradi na kuhakikisha halmashauri hiyo inafikia lengo walilojiwekea kwenye ukusanyaji wa mapato na utoaji wa huduma kwa Wananchi.

Akiongea wakati wa ugawaji pikipiki hizo kwa Watendaji wa Kata hizo Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Edward Mpogolo aliipongeza Halmashauri ya Same kwa kutenga fedha na  kununua vitendea kazi hivyo kwa Watendaji. Nakuahidi kusimamia Watendaji hao kuzitumia pikipiki hizo Katika kusudi yaliyolengwa.

Mpogolo amesema Watendaji waliokabidhia wahakikisha wanajifunza kuendesha pikipiki na kupata leseni na hata mfumbia macho Mtendaji yeyote atakaye badilisha matumizi ya pikipiki hizo kama walivyoagizwa.

"Nikweli wenzetu wa halmashauri wametoa fedha kwaajili ya kununua pikipiki hizi kwa Watendaji wetu wa Kata 16 lengo ni kufikia kata zote 34 kwenye Halmashauri yetu na kuwa mfano bora wa kusimamia Maendeleo na kutoa huduma kwa Wananchi wetu wa Same. "Amesema Mpogolo"

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo ya Same Annastazia Tutuba akitoa taarifa ya ununuzi wa pikipiki hizo amesema wametumia kiasi cha milioni 43.6 kununua pikipiki hizo 16 na katika pesa hizo kiasi cha milioni 6 zimetumika kununua pikipiki ya magurudumu matatu (Guta) kwaajili ya shughuli mbalimbali za mamlaka ya mji mdogo wa Same.

Tutuba amesema lengo la halmashauri ni kuwajengea mazingira rafiki ya ukusanyaji wa mapato Watendaji wake wa Kata ilikuongeza ufanisi na kufikia malengo waliojiwekea ya ukusanyaji wa mapato wa kiasi cha bilioni 2.5 kwa mwaka wa fedha 2021-2022.

"Tumeona ni vyema kuwanunulia pikipiki Watendaji wetu hawa wa Kata 16 ilikuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato kwenye Kata zao na ukiangalia Kata tulizopeleka pikipiki hizi ni zile zenye changamoto ya usafiri na nyingi niza milimani"Amesema Tutuba.

Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, Edward Mpogolo (wa pili kushoto) akikabidhi Pikipiki kwa mmoja wa watendaji wa kata wa Wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, Edward Mpogolo akiwa amepanda moja ya Pikipiki ambazo amezikabidhi kwa watendaji wa Kata 16 kwenye Wilaya hiyo.
Baadhi ya Pikipiki ambazo Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, Edward Mpogolo amezikabidhi kwa watendaji 16 wa Wilaya hiyo.
 
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2