DKT. CHAULA ATOA RAI KWA VIJANA KUTUMIA TEHAMA KUTAFUTA FURSA | Tarimo Blog

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula akifungua mafunzo ya siku nane kwa wanafunzi 50 wa taasisi za elimu ya juu wanataaluma wa TEHAMA yanayotolewa na Kampuni ya HUAWEI Tanzania kupitia program yao ya Seeds for the future jijini Dodoma.



Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula akimtunuku cheti cha ushiriki wa mafunzo ya siku nane, moja ya wanafunzi 50 wa taasisi za elimu ya juu wanataaluma wa TEHAMA yanayotolewa na Kampuni ya HUAWEI Tanzania kupitia program yao ya Seeds for the future jijini Dodoma. Kulia ni Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha Dodoma Profesa Faustine Bee na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Huawei Tom Tao.



Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha Dododma Profesa Faustine Bee akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya siku nane kwa wanafunzi 50 wa taasisi za elimu ya juu wanataaluma wa TEHAMA yanayotolewa na Kampuni ya HUAWEI Tanzania kupitia programu yao ya Seeds for the future jijini Dodoma


Mkurugenzi Msaidizi wa HUAWEI Tanzania Tom Tao akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya siku nane kwa wanafunzi 50 wa taasisi za elimu ya juu wanataaluma wa TEHAMA yanayotolewa na Kampuni ya HUAWEI Tanzania kupitia programu yao ya Seeds for the future jijini Dodoma



Baadhi ya washiriki na uzinduzi wa programu ya HUAWEI ya Seeds for the future wakifuatilia hotuba fupi iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (hayupo pichani ) wakati akizundua program hiyo jijini Dodoma.



Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula (walioketi wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wakufunzi na wataalamu walioshiriki uzinduzi wa programu ya HUAWEI Tanzania ya Seeds for the future jijini Dodoma. Kulia ni Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha Dodoma Profesa Faustine Bee, wa tatu kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa HUAWEI Tanzania Tom Tao, wa pili kushoto waliosimama ni Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA wa Wizara hiyo Mulembwa Munaku.



Na Faraja Mpina, Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainabu Chaula ametoa rai kwa vijana kutunza maadili ya nchi na kuwa na matumizi sahihi ya teknolojia kwa maslahi mapana ya nchi kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano kutafutia fursa za kiuchumi na kupata taarifa sahihi za biashara, elimu na afya

Dkt. Chaula amezungumza hayo wakati akizindua mafunzo ya siku nane ya programu ya HUAWEI Tanzania iitwayo Seeds for the future jijini Dodoma leo tarehe 03 Septemba 2021

Ameizungumzia programu hiyo kama fursa ya kuongeza uwezo na kukuza vipaji kwa vijana wanataaluma wa TEHAMA kupitia kampuni ya HUAWEI ambao ni wadau muhimu wa Sekta ya Mawasiliano katika kuweka mazingira wezeshi ya kukuza TEHAMA nchini

Amesema kuwa programu hiyo kwa mwaka huu inawahusisha vijana 50 ambao ni wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu watakaopata nafasi ya kujifunza teknolojia za kisasa za TEHAMA zitakazokuza uwezo na ubunifu wao na kuwaletea faida wao binafsi, Taifa na jamii kwa ujumla

Aidha, Dkt. Chaula amesema kuwa fursa nyingi zinapatikana kupitia TEHAMA na kati ya vijana 50 watakaopatiwa mafunzo hayo vijana 40 ni wasichana kitu ambacho kinatia moyo na kutoa hamasa kwa vijana hasa kutokana na ushuhuda wa moja ya wanufaika wa programu hiyo Bi. Emilina Masanja kutoka chuo kikuu cha Mzumbe aliyesema kupitia TEHAMA amekuza biashara yake kwa kuongeza wigo wa wateja ambao wengine wapo nje ya nchi

Naye Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dodoma Profesa Faustine Bee amesema kuwa chuo hicho kina ndaki ambayo inafundisha taaluma ya teknolojia ya habari na mawasiliano inayoitwa CIVE, hivyo programu ya HUAWEI Tanzania ya Seeds for the Future inatoa hamasa kwa vijana wanaochukua kozi za TEHAMA kwa kuwapa nafasi ya mafunzo kwa vitendo na pia inawezesha vijana hao kuweza kujiajiri na kuajirika

Henry materu kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam ni moja ya wavulana 10 waliochaguliwa kujiunga na programu hiyo amesema mategemeo makubwa ya program hiyo ni kuleta matokeo chanya katika mawanda ya teknolojia kwasababu juhudi nyingi zinafanyika za kukuza sekta ya mawasiliano nchini

Kwa upande wa Mkurugenzi Msaidizi wa HUAWEI Tanzania Tom Tao amesema kuwa mafunzo hayo ni yameanza kutolewa mwaka 2016 kwa kuchagua wanafunzi 10 wa TEHAMA wanaofanya vizuri kutoka katika taasisi za elimu ya juu kwa kuwapatia mafunzo ya teknolojia za kisasa katika TEHAMA nchini China na pia kujifunza utamaduni wao

Ameongeza kuwa kutokana na changamoto za UVIKO 19, kuanzia mwaka jana mafunzo hayo yamekuwa yakitolewa kwa njia ya mtandao na idadi ya wanafunzi hao kuongezeka kutoka 10 hadi kufikia wanafunzi 50 ambapo mpaka sasa jumla ya wanafunzi 150 wamenufaika na programu hiyo

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2