Mchengerwa alia na matapeli wanaowatapeli watumishi wa umma. | Tarimo Blog


*Ataka wataofanyiwa jaribio la utapeli kutuma kwenye namba ya TCRA 15040


Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa amewatahadharisha Watumishi wa Umma, Watumishi wastaafu na wananchi kwa ujumla kutokutoa fedha au taarifa zao kwa watu ambao  wanadhaniwa  kuwa ni matapeli hivyo kuwataka kutoa taarifa katika ofisi husika ili waweze kushughulikiwa.

.Mchengerwa amesema hayo l alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JINCC) Jijini Dar es Salaam,amesema taratibu za kutatua changamoto za watumishi zipo katika utaratibu na sio vinginevyo.

Mchengerwa amesema matapeli hao wanatumia mwanya huo kutokana na baadhi ya maeneo kuwepo kwa ulasimu na kuwataka watendaji wa umma kufanya kazi kwa weledi katika kutatua changamoto.

Aidha .Mchengerwa ametoa onyo kwa wale wote ambao wanajihusisha na uhalifu huo kuacha mara moja kwani Serikali kupitia vyombo vyake inaendelea kufuatilia taarifa hizo kwa ukaribu ili kuweza kuwabaini matapeli hao na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

"Niwaombe Watumishi wa Umma na wananchi kwa ujumla wenye taarifa za mtu yeyote wakiwemo Watumishi wa Umma wanaojihusisha na vitendo vya kiharifu vya namna hii kuleta taarifa zao sehemu husika". Amesema Waziri Mchengerwa.

Amesema Watumishi wa Umma watakaopigiwa simu na matapeli na kuombwa kutoa fedha au taarifa zao ili waweze kushughulikiwa masuala yao wawasilishe namba za simu zilizotumiwa na waharifu hao katika Mamlaka za Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia namba ya simu 15040.

Sambamba na hayo Waziri Mchengerwa amewataarifu wananchi na Watumishi wa Umma kuwa endapo watahitaji ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya kiutumishi wapige simu katika kituo cha mawasiliano cha ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa namba ya simu 0262160240 au kwenye kituo cha mawasiliano cha Ofisi ya Rais TAMISEMI kupitia namba ya simu 0262160210.

Mchengerwa amewataka watumishi wa Umma katika maeneo yao ya kazi kuhakikisha wanaondosha urasimu na kutoa nafasi ya kuwasikiliza wananchi na kutatua  kero zao.

"Niwaombe viongozi walioteuliwa na kuchaguliwa wawasikilize wananchi na kuweza kutatua kero zao na kuepusha urasimu katika ofisi zao ili kutoa fursa kwa watanzania kupeleka kero zao na malalamiko yao waweze kuwasikiliza na kupata ufumbuzi kuhusu kero zao kwani ongezeko la urasimu popote mahala pa kazi hutengeneza mazingira ya kiutapeli na kutoa nafasi kwa watu wasio wema kutumia fursa hiyo kufanya utapeli kwa Watumishi na wananchi kwa ujumla katika mazingira yao". Amesema Mhe.Mchengerwa.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya  Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mohamed Mchengerwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na matapeli kwa watumishi wa umma kuombwa fedha ,jijini Dar es Salaam.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2