WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako (Mb) Septemba 3, 2021 Jijini Dar es Salaam amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Simai Mohammed Said kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Sekta ya elimu ikiwemo kuendeleza ushirikiano katika kutoa Elimu bora Nchini.
Akizungumza katika kikao hicho Waziri Ndalichako amesema ni vizuri kuendeleza misingi ya ushirikiano katika masuala ya Elimu ikiwa ni kudumisha Muungano na kwa pamoja kuendelea kutoa wahitimu wenye ujuzi stahiki kulingana na mahitaji ya Taifa kwa ujumla.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Simai Saidi baada ya mazungumzo ya pamoja kuhusu masuala ya elimu yaliyofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akipokea zawadi ya Kitabu kutoka kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Simai Saidi alipofika ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam kufanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya elimu.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment