Na Linda Shebby , Bagamoyo
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka wakazi wa eneo la Kata ya Zinga Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani kuendelea kuwa wastahmilivu kwani mambo mazuri yanakuja kutoka kwa serikali ambapo kila muhusika atapata stahili zake ili waweze kupisha uwekezaji wa mradi wa Bandari.
Mheshimiwa Rais Samia ameyasema hayo leo subuhi aliposimama katika eneo hilo la Zinga Bagamoyo aliposimama na kuwasalimia wananchi wa eneo hilo wakati alipokuwa akielekea Bagamoyo kwa ziara yake ya kikazi ya kutangaza utalii wa nchi inayoendelea.
Akizungumza kuhusu masuala ya Bagamoyo kuhusu mpango wa mradi wa bandari alisema kuwa serikali hivi sasa inaondoa vipengele ambavyo vilikwamisha mradi huko nyuma na kuwa hivi sasa serikali wanaupitia kama serikali tunawahakikishia , kuwa miradi yote ambayo ilianza inamalizika huku akisema kuwa pia kutaanzishwa miradi mingine.
"Mradi ule utaleta maendeleo mbalimbali ikiwemo, kufikisha maji, umeme kila sehemu ya Bagamoyo Ili kuwanufaisha wakazi wa eneo husika"alisema Rais.
Alisema tozo zitaendelea kwa sababu misaada imepungua kwa kiasi kikubwa hivyo amewataka wananchi kuwa watulivu kwani vyanzo vya mapato vimepungua hivyo tumeamua kuchangishana Ili kujena madarasa na vituo vya afya na ni wajibu wa wananchi kuchangishana Ili kuweza kuendeleza miradi mbalimbali ya ndani.
Aidha akizungumzia kuhusu suala la ugonjwa wa Uviko 19 alisema ugonjwa huu upo ila hawezi kumlazimisha mtu kuchanja huku akisisitiza kuwa kuchanja ni hiari ya mtu binafsi.
Alisisitiza kuwa tozo zitaendelea kwa kuchangishana na kusema kuwa umefika muda wa wananchi kuchangia na fedha zitakazofanyika zijengwe Shule na hospital kelele za mlango hazimuachishi mwenyemba kulala.
"Mradi ule utaleta maendeleo kwa wananchi pamoja na kutoa ajira kwa vijana wote wa Bagamoyo pia utaondoka changamoto zote za njia"alisema Mh.Rais Samia Suluhu Hassan.
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan aliyasema hayo alipokuwa akijibu hoja iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge kuhusiana na sintofahamu iliyokuwa miongoni mwao juu ya malipo ya fidia ya maeneo yao Ili kupisha uwekezaji wa Bandari.
Eneo hili ni eneo ambalo linatarajia kujengwa bandani kubwa ya Bagamoyo pamoja na uwanja wa Ndege miradi ya EPZAna Maeneo makubwa ya uwekezaji yenye ukubwa wa Hekta 6800.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge amemuomba Mheshimiwa Rais Samia kuagiza kuwekwa taa zitakazowaka muda wote ikiwa ni katika kukuza utalii katika Wilaya ya Mafia ambapo hali hiyo itasaidia kukuza utalii kisiwani humo.
"Kisiwa Cha Mafia tunaomba Uwanja wa Ndege uwekwe taa Ili Ndege ziweze kutua muda wote itasaidia kukuza utalii kwani Kuna maji ya bluu na mchanga mweupe na mazingira yake yanafanana na Zanzibar" alisema RC Kunenge.
RC Kunenge aliongeza kwa kusema kuwa anamuomba Mheshimiwa Rais Samia kujenga barabara ya Kisarawe kwenda Rufiji kwa sababu itasaidia kufungua njia kwa watalii ndani ya Mkoa na wanachi kwenda kwa urahisi katika mbuga ya Selou hivyo sekta ya utalii itakua Mkoani Pwani.
"Akizungumza mzia suala la Hali ya Usalama wa Mkoa wa Pwani alisema hivi sasa hali ni tulivu"alisema RC Kunenge
Naye Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani Subira Mgalu ametoa shukran zake za dhati kwa niaba ya wanawake wa Mkoa huo ikiwemo kuanzishwa kwa miradi ya maji inayoendelea kimkakati.
Alisema " Kwa Mara ya kwanza Mkoa wa Pwani tumempokea Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kikubwa mimi kama mwakilishi wa wanawake Mkoa wa Pwani nasema tunamshkuru kwani tumeanza kuona faida ya miamala ya simu kwani zaidi ya vituo vinne vya afya kwa tarafa nne Mkoani Pwani Bagamoyo vimefaidika kwa kupitia tozo hizo pia nampongeza kwa kufanya mapitio na kupunguza gharama za tozo hizi hivyo Watanzania waelewe umuhimu wa kuchangia tozo hizo.
"Niungane na wabunge wenzangu nikushukuru pia kwa ajili ya miradi ya maji yakimkakati inayoendelea ambayo ipo mkoani Pwani na ulishakuja kuitembelea" alisema Mheshimiwa Mgalu .
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete katika mkutano huo kwa niaba ya wananchi wa jimbo la Chalinze alikumbushia ahadi ya Hayati Rais John Magufuli ya kupandisha hadhi jimbo la Chalinze kuwa Wilaya ili kusogeza huduma za jamii karibu na wananchi.
Mheshimiwa Ridhiwani alisema wananchi wanatembea umbali mrefu kutoka maeneo ya vijijini kuja Bagamoyo mjini kufuata huduma zinazotolewa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Alisema "kwa mfano wananchi wa kutoka Kata ya Kibindu wanatembea umbali mrefu sana wa kilomita zaidi ya 300 kuja Bagamoyo mjini kumwona Mkuu wa wilaya kufuata huduma lakini huduma hizo zitakuwa karibu iwapo Chalinze itakuwa wilaya ambapo wananchi watahudumiwa kule kule Chalinze hata huduma za mahakama" alisema Mheshimiwa Ridhiwani.
"Mimi nikuombe sana sana Mama ukiwa ni Rais wetu, kipenzi chetu ulifanyie kazi na sio kwamba tunataka tuwakimbie wanabagamoyo bali Chalinze ikiwa Wilaya itawapunguzia sana gharama wanachalinze katika kupata huduma" alisema Ridhiwani.
"Ukitupatia Mkuu wa wilaya kule kule Chalinze mambo yetu yatakwenda vizuri" alisema.
Hatahivyo Mbunge wa jimbo la Bagamoyo Mheshimiwa Muharami Mkenge aliomba kujengwa kwa Ghati ya boti za kasi Bagamoyo itakayounganisha na kurahisisha safari za watalii kuja na kurudi Zanzibar baada ya kutegemea bandari ya Dar es salaam.
Mkenge alisema kutokana na ukaribu wa Bagamoyo na Zanzibar watalii wanaweza kuja na kurudi Zanzibar kwa muda mfupi hivyo ghati hiyo itaimarisha uchumi wa nchi kupitia utalii nchini.
Alisema watalii wengi wanashindwa kufika Bagamoyo kutokana na kukosekana kwa ghati itakayorahisisha muda na kupunguza umbali kwa watalii.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment