Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kutoa elimu ya namna ya kuhakikisha usalama na ubora wa bidhaa za Muhogo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga. | Tarimo Blog

Afisa Udhibiti Ubora TBS, Bi.Ashura Kilewela akitoa elimu namna ya kuhakikisha usalama na ubora wa bidhaa za Muhogo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga.



Akizungumza katika mafunzo hayo, Afisa Udhibiti Ubora TBS, Bi.Ashura Kilewela amesema pamoja na umuhimu wa zao la muhogo kwa chakula, zao hilo huathiriwa na kemikali ya sumu asili (Natural toxin) ambayo hutokana na uwepo wa kemikali inayozalishwa na mmea wenyewe inayoitwa  Sianidi.

"Kiasi cha kemikali ya sianidi katika muhogo hutofautiana kutegemea na aina ya muhogo husika na ladha yake. Kuna muhogo mtamu, aina hii ya muhogo ina ladha tamu na kiasi kidogo cha kemikali ya sianidi, pia kuna muhogo michungu, muhogo hii ina ladha chungu na ina kiasi kikubwa cha kemikali ya sianidi". Amesema Bi.Ashura.

Amesema inafahamika aina ya udongo huchangia kuongezeka au kupungua kwa Sianidi katika muhogo.Kipaumbele kimewekwa kwenye athari za kilimo zisizo sahihi, uchakataji na usindikaji wa muhogo huchukua miezi 8-12 hadi muda wa kuvuna na mingine hadi miezi 24.

Aidha Bi.Ashura amesema mlaji anaweza kupata madhara ya kiafya yatokanayo na sumu asili aina ya sianidi endapo atakula chakula kitokanacho na muhogo chenye kiasi kikubwa cha kemikali hiyo. Chakula hicho kinaweza kuwa muhogo uliomenywa na kuliwa mbichi, kupikwa, bidhaa zitokanazo na muhogo au majani yake (kisamvu).

"Madhara ya sianidi yanaweza kutokea baada ya muda mfupi au mrefu kutegemea na kiasi cha kemikali hiyo kwenye chakula kilicholiwa , umri na hali ya afya ya mlaji". Ameeleza Bi.Ashura.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2