Na Victor Masangu,Pwani
Mkuu wa Mkoa wa Pwani amewataka wakandarasi wa walioingia mkataba kwa ajili ya kutekeleza miradi 17 ya maji katika yenye thamani ya bilioni 7.8 maeneo ya vijijini kutokuwa na visingizio vya mvua na badala take wafanye kazi kwa kujituma ili wawe kumaliza miradi hiyo kwa muda uliopangwa ambao wa miezi sita.
Kunenge ametoa kauli hiyo wakati wa halfa fupi ya utiaji saini wa mikataba kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji kupitia Mpango wa maendeleo na ustawi wa Taifa iliyofanyika Mjini Kibaha ambayo ilihudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali wakandarasi,viongozi wa Chama pamoja na baadhi ya Wabunge wa mkoani Pwani.
Katika halfa hiyo Mhe.Kunenge aliwaasa wakandarasi hao wote ambao wamesaini mikataba kuhakikisha wanaijenga katika kiwango kinachotakiwa ili iwezekudumu kwa kipindi Cha muda mrefu.
"Kikubwa ninachokiomba kwa wakandarasi wote ambao wamepewa dhamana hii ya kutekeleza miradi ya maji kujjtahidi kuijenga katika ubora na sio iwe katika kiwacho Cha chini na kupelekea miundombinu mingine ikiwemo mabomba kuvuka maji kwa hivyo vifaa vinavyotumika inapaswa viwe vya uhakika,"alisema Kunenge.
Kadhalika Kunenge alibainisha kuwa kuna baadhi ya wakandarasi wengine wanachelewesha kumaliza kwa wakati miradi mbali mbali katika maeneo na Pwani kwa visingizio mbali mbali ikiwemo mvua kunyesha hivyo wanapaswa kubadilika ili ndani ya kipindi Cha miezi sita wananchi waweze kupata huduma ya maji.
"Wakandarasi nyie mmekubalika na mmekidhi vigezo mnapaswa kukamilisha miradi hii kwa wakati kwani Jografia mmnaijua hatutapenda kuona kuna sababu labda zile za majanga kwani mvua siyo sababu kubwa kwa hivyo hili mliangalie kwa makini,"alisema Kunenge
Aidha katika hatua nyingine aliahidi kuendelea kuwapa ushirikiano wa kutosha wakandarasi wote lengo ikiwa ni,serikali kujitahidi kutoa fedha kwa ajili ya kupunguza ama kuondoa changamoto ya maji kwa wananchi wote hasa wa maeneo ya vijijini.
Alisema , fedha zilizotolewa kwenye bajeti ya mwaka 2021 serikali ilitoa fedha kiasi cha sh.bilioni 12 sawa na asilimia 41 na zimeongezeka kufikia bilioni 21 sawa na asilimia 76 kwa bajeti ya mwaka 2022 hali ambayo itaongeza upatikanaji wa huduma ya maji Safi na salama.
Kwa upande wake Meneja waWakala wa maji na usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) Mkoa wa Pwani Mhandisi Beatrice Kasimbazi alisema kuwa miradi hiyo ni ya awamu kwanza na itatekelezwa kwenye Halmashauri za wilaya zote za mkoa wa Pwani.
Kasimbazi alisema kuwa kupitia miradi hiyo fedha zake zinatokana na Mpango wa maendeleo wa ustawi wa Taifa wa mapambano dhidi ya Covid-19 kiasi cha shilingi bilioni 2.6 Mango wa malipo kwa Matokeo (PbR) 445.4 na Mfuko wa maji bilioni 4.7.
Alisema kuwa bajeti kuu ya mkoa kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 ulitengewa kiasi cha shilingi bilioni 21.4 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji Vijijini.
Kasimbazi alisema kuwa fedha hizo zimetokana na Mapambano dhidi ya Covid -19 bilioni 3.7 Mfuko wa maji (NWF) na serikali kuu bilioni 15.2 na Malipo kwa Matokeo (PbR) bilioni 2.4 na ikikamilika itawafikia wakazi 102,307.
Naye mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani Ramadhan Maneno alisema kuwa watahakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati kwa kuitembelea ili kuona mwenendo wake ili kuwapunguzia kero za maji wananchi.
Naye mwenyekiti wa wabunge wa mkoa wa Pwani Muharami Mkenge alibainisha, upatikanaji wa fedha hizo zitasaidia kukabiliana na changamoto za maji kwenye mkoa huo.
Nao baadhi wa wakandarasi ambao wameweza kupata fursa ya kusaini mikataba hiyo wameahidi kuyatekeleza maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa na kwamba watachapa kazi usiku na mchana ili kuendana na muda uliopangwa.
Baadhi ya picha mbalimbali katika halfa ya utiaji wa saini mkataba wa kutekeleza miradi 17 ya maji ambayo inasimamiwa na RUWASA.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment