Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui TCRA, Hans Gunze akitoma maamuzi ya Kamati ya Maadili ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) leo Desemba 17,2021 dhini ya kesi ya Maudhui ya Kimtandao iliyokuwa ikimkabiri Mbunge Hamfrey Polepole kupitia Televisheni yake ya Mtandaoni ya Hamfrey Polepole Tv kupitia Kipindi cha Shule ya Uongozi.
Baadhi ya wanakamati ya Kamati ya Maadili ya TCRA wakati wa Mwenyekiti wa Tume hiyo akisoma maamuzi ya Kesi ya Maudhui ya Mtandaoni.
Mbunge Hamfrey Polepole akizungumza mara baada ya Kusomewa maamuzi ya TCRA leo Desemba 17,2021 jijini Dar es Salaam.
*Ni kitokana na kukiuka masharti ya leseni chini ya Mwendeshaji Hamphrey Polepole
Na Avila Kakingo,Michuzi TV
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekisimamisha kipindi cha Shule ya Uongozi kinachorushwa na Televisheni ya Mtandaoni ya Hamphrey Polepole.
Akizungumza wakati wa kutoa maamuzi ya Kesi ya Televisheni ya Mtandaoni ya Hamphrey Polepole leo Desemba 17,2021 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui TCRA, Hans Gunze amesema kuwa Televisheni hiyo imekiuka sheria, Kanuni, Misingi na maadili ya waandishi na utangazaji wa habari pamoja na masharti ya leseni yake.
Pamoja na adhabu hiyo Kituo hicho kimepewa onyo kali huku kikiamriwa kutoa taarifa TCRA na Mamlaka hiyo ikijiridhishi, kipindi hicho
kinachorushwa na Televisheni ya mtandaoni kitarejea na kuwa chini ya Uangalizi wa Mamlaka hiyo kwa kipindi cha Miezi sita.
Gunze amesema kuwa haki ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo kwenye baraza la ushindani na haki kibiashara upo wazi ndani ya siku 21.
Uamuzi huo umekuja mara baada ya Kituo hicho cha Televisheni Mtandaoni kutoa habari mbalimbali zinazopotosha umma na zinazoweza kusababisha wananchi kugomea kampeni ya kitafa ya kujikinga na virusi vya Corona.
Aidha Gunze amesema kuwa Oktoba 21, 2021 kituo hicho cha Televisheni kupitia kipindi cha shule ya uongozi kimetuhumiwa kukiuka sheria kwa kutangaza habari yenye viashiria vya uchonganishi kati ya wananchi na viongozi wa Serikali juu ya suala la tamko la Rais Samia Suluhu Hassan kwa wakuu wa Mikoa nchini kuwapanga wafanyabiashara wadogo wa dogo (Machinga).
Kwa Upande wake Mbunge Hamphey Polepole amesema kuwa kazi ya Kusema ukweli inasafari kidogo. Amesema atakaa na kutafakari Maamuzi yaliyotolewa na kamati ya maadili ya TCRA na atatoa taarifa kwa hatua inayofuata.
"Kazi ya Kusema kweli bado ni asafari na mimi sitakata tamaa maadamu ninachokifanya kinalenga maslahi mapana ya nchi yetu ya Tanzania na watu wake, Mamlaka ya nchi na Chama Chetu Cha Mapinduzi." Alimalizia Polepole.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment