UVCCM ILEJE KUWASHUGHULIKIA WANAOBEZA SHUGHULI ZA RAIS SAMIA | Tarimo Blog


Na Denis Sinkonde_Songwe.

Mwenyekiti wa umoja wa vijana(UVCCM) wilaya ya ILeje mkoani Songwe Maoni Jeckison Mbuba amewataka vijana kumuunga mkono Rais Samia

Akifungua kikao Cha baraza la kawaida la umoja wa vijana lililofanyika Disemba 29, 2021, Mbuba amesema rais Samia ametambua uhitaji wa wananchi ikiwepo sekta ya Afya, Elimu na maji hivyo wananchi wanapaswa kumuunga mkono ili kufanikisha azma ya Taifa hili.

Mbuba amesema baadhi ya wanaccm hubeza juhudi za mweshimiwa Rais hivyo kama jumuiya Haina budi kuisemea serikali kwa mambo inayotekeleza kuwapelekea wananchi maendeleo kwa kuzingatia Ilani ya chama Cha mapinduzi.

''Wanaccm wanapaswa kuisemea vyema serikali kwa utekelezsjo wa mradi ya maendeleo katika maeneo Yao ikiwepo usimamizi wa ujenzi wa hospitali, vituo vua Afya ,miradi ya maji na ujenzi wa vyumba vya madarasa unaendelea nchi nzima ili wananchi wapate huduma hizo kwa ukaribu alisema Mbuba".

Baadhi ya wajumbe wa baraza la umoja wa vijana ccm wilaya ya ILeje kutoka kata 18 zinazounda wilaya ya Ileje wamesema hawatasita kuwachukulia hatua watu wanaobeza juhudi za rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza miradi ya maendeleo

Katibu wa chama Cha mapinduzi wilayani humo Hassan Lyamba amewataka vijana hao kudumisha amani , upendo na mshikamano iliyoachwa na waasisi wetu akiwepo baba wa taifa hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Siasa zisiwe chanzo Cha kuvunja amani Bali iwe sehemu ya kueneza amani kwa lengo la kuepusha matukio ya uhalifu hususani wilaya ya ILeje ikiwa sehemu ya nchi ya Tanzania ikipakana na nchi za Malawi na Zambia ''alisema Lyamba".





Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2