UWT wilaya ya Njombe watekeleza agizo la kuwa na nyumba za watumishi | Tarimo Blog

Na Amiri Kilagalila,Njombe
JUMUIYA ya umoja wa wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Njombe,imefanikiwa kutekeleza agizo la Chama ngazi ya taifa kwa kujenga nyumba za watumishi ili kupunguza changamoto za watumishi wa Jumuiya wanapokuwa wamepanga mitaani.

Akizungumza baada ya kukagua nyumba hiyo iliyopo mtaa wa Nzenge halmashauri ya mji wa Njombe,Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe Scolastika Kevela,amesema jumuiya hiyo wilaya ya Njombe imeonyesha mfano kwa wilaya zote za mkoa huo na taifa kwa kutekeleza agizo kwa wakati na kuahidi kuendelea kumuunga mkono mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi taifa kwa vitendo.

“Kwanza niwapongeze UWT wilaya ya Njombe kwa kazi kubwa mliyoifanya,hili ni agizo kutoka taifa kwamba tuhakikishe mkoa na wilaya zote tunajenga nyumba za watumishi wa jumuiya ili kupunguza changamoto za kupanga”alisema Scolastika Kevela

Ameongeza kuwa mkoa wa Njombe utaenedelea kuwa bega kwa bega na mwenyekiti wao wa Chama taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

“Njombe tuko bega kwa bega na Samia Suluhu na 2025 Njombe tutakuwa na jambo letu na tutaendelea kumuunga mkono kwa vitendo na huu ndio utendaji unaoonekana”alisema Kevela

Naye mwenyekiti wa jumuiya hiyo wilaya ya Njombe Betrece Malekela,amesema agizo hilo lilitolewa tarehe 23 ya mwezi wa 9 wakiwa Rufiji na kupata hamasa kubwa ili kumailisha nyumba hiyo kwa wiki tatu pekee na kuwa miongoni mwa wilaya chache nchini zilizotekeleza agizo hilo.

“Tulipata hamasa na tukatii maagizo maana ilionekana ni nyumba chache zilizojengwa kwa nchi nzima,nyumba hii imekamilika ndani ya wiki tatu wala sio kitu kidogo”alisema Betrece Malekela

Wajumbe wa baraza la UWT mkoa wa Njombe waliofika na kukagua nyumba hiyo,wamesema ukamilishaji wa nyumba hiyo umetokana na umoja walio nao na wilaya ya Njombe imekuwa ni mwanga na kutoa hamasa kwa wilaya nyingine kutekeleza agizo hilo.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe Skolastika Kevela pamoja na wajumbe wa baraza wakikagua idadi ya vyumba na muonekano wa ndani wa nyumba hiyo iliyopo mtaa wa Nzenge.
Muonekano wa upande wa nyumba ya kisasa ya jumuiya ya UWT wilaya ya Njombe iliyojengwa kwa ajili ya katibu wa jumuiya hiyo ili kupunguza changamoto za kupanga mitaani.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

3/Post a Comment/Comments

Post a Comment

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2