WAHIFADHI WA TFS KANDA YA MASHARIKI WAVISHWA VYEO | Tarimo Blog

 Ukiwa ni muendelezo wa Mkakati wa kuhakikisha kwamba Wahifadhi wa TFS wanatambulika kwa Vyeo vyao stahiki vya Jeshi la Uhifadhi, jumla ya Wahifadhi 49; Maafisa 15 na Askari 34 toka Vituo vya TFS vilivyopo katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, Kanda ya Mashariki walivishwa vyeo. Zoezi hilo lilifanyika Jana Tarehe 30 Desemba, 2021 katika Viwanja vya Ofisi za Shamba la Miti Ruvu Kaskazini zilizopo Kongowe Wilayani Kibaha. 


Hafla hiyo, ilihudhuriwa na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Caroline Malundo ambaye ni Kamanda wa Kanda ya Mashariki aliyekuwa Mgeni Rasmi akimuwakilisha Kamishna wa Uhifadhi TFS Profesa Dos Santos Silayo. Lengo ni Wahifadhi kutambulika kwa Vyeo vyao stahiki ili kutekeleza majukumu ya Uhifadhi na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Misitu na Nyuki ipasavyo. "Malundo"








Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2