Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
HALMASHAURI Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bukombe mkoani Geita imempongeza Mwenyekiti wa chama hicho Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Akitoa pongezi hizo kwa niaba ya wajumbe wa Halmashauri hiyo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukombe Daniel Machongo amesema Rais Samia anastahili pongezi kubwa kwa kuwa ameendelea kuisimamia vyema nchi licha ya kuipokea katika kipindi cha majonzi makubwa.
Machongo ametumia fursa hiyo kumuombea afya njema Rais Samia ili azidi kuwaletea wananchi maendeleo huku akisema kuwa Halmashauri Kuu wa CCM Wilaya ya Bukombe iko naye bega kwa bega.
Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai hadi Disemba 2021, Mkuu wa Wilaya Bukombe Said Nkumba alieleza kuwa Wilaya hiyo ilipokea zaidi ya shilingi bilioni mbili kupitia fedha za UVIKO 19 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na mindombinu yake hatua ambayo imeondoa uhaba uliokuwepo katika Shule za Msingi na Sekondari.
Naye Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko amesema Rais Samia ana mapenzi ya dhati na Wilaya ya Bukombe na Taifa kwa ujumla ndiyo maana amezidi kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kwamba huo ni mwanzo tu kwani mambo makubwa zaidi yanakuja.
Wajumbe wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya Bukombe wakifuatilia taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020/25 kipindi cha Julai hadi Disemba 2021 ambapo pamoja na mambo mengine walimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuiongoza vyema nchi.
Mkuu wa Wilaya Bukombe, Said Nkumba pia aliwapongeza waalimu na wadau wa elimu wilayani Bukombe kwa kazi nzuri iliyowezesha ufaulu kwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko akitoa salamu kwenye kikao hicho ambapo aliwahimiza wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilayani Bukombe kuwa wamoja ili kusukuma gurudumu la maendeleo kwa pamoja.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko alimshukuru Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyowajali wananchi na kuelekeza fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa mirai ya maendeleo.
Wajumbe wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Bukombe wakifuatilia kikao hicho.
Tazama Video hapa chini
SOMA>>> Habari zaidi kutoka Bukombe
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment