Na Khadija Seif, Michuziblog
TAASISI ya Kusaidia watu wenye uhitaji Happy Hands Tanzania wahaidi kuendeleza juhudi za Kumuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutangaza utalii wa ndani.
Happy hands Wamedhamiria Kwa dhati kuunga Mkono juhudi hizo Kwa Kumleta Mwanamuziki kutoka nchini Sweden Mahir zein hapa Tanzania na kumpelekea katika Moja ya hifadhi za Wanyama katika Mkoa wa Arusha pamoja na Visiwa vya Zanzibar.
Hata hivyo Mahir zein atakuwepo nchini Kwa lengo la kutoa burudani mapema mwezi Marchi 12 na kutembelea vivutio vilivyopo nchini kabla ya tarehe rasmi ya Tamasha hilo anatarajiwa kutembelea Mbuga za wanyama zilizopo Arusha.
Hata hivyo taasisi hiyo Kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imempa nafasi Mwanamuziki huyo kutembelea vivutio vilivyopo Visiwa vya Zanzibar.
Mahir zein anatarajiwa kutumbuiza katika Ukumbi wa Dom uliopo Masaki jijini Dar es salaam na viingilio ni shilingi elfu 50.
Aidha, Happy Hands imeomba wadhamini kujitokeza Kwa wingi katika kufanikisha Tamasha hilo na Kwa mwaka huu mikakati Yao ni kuendelea kusaidia wanawake,walemavu pamoja na watoto Kwa kiasi kitakachopatikana katika Tamasha hilo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment