VIONGOZI mbalimbali pamoja na wananchi wanaendelea kutembelea Maonesho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika katika Viwanja vya Nyerere ‘Square’ jijini Dodoma yalioanza tarehe 23 Januari, 2022. Ikiwa ni siku ya tano ya Maonesho haya, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Jumanne Sagini naye alipata nafasi ya kutembelea maonesho hayo jana tarehe 27 Januari, 2022 yanayofanyika katika viwanja tajwa.
Mhe. Sagini ameipongeza Mahakama ya Tanzania kwa Maonesho mazuri yaliyopangiliwa vizuri huku akitoa rai kuitangaza zaidi wiki ya sheria ili wananchi wengi zaidi waweze kunufaika na maonesho hayo.
Matukio katika Picha-Ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi katika Maonesho ya Wiki Ya Sheria Nchini
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Jumanne Sagini (kulia) akizungumza jambo na Maafisa kutoka Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ambapo alipata nafasi ya kutembelea banda hilo jana tarehe 27 Januari, 2022. Aliyeshika Kipaza sauti 'mic' ni Bi. Dorothy Moses, Msajili Msaidizi wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya. Maonesho ya Wiki ya Sheria Nchini yatahitimishwa tarehe 29 Januari, 2022 na kilele chake kitakuwa tarehe 01 Februari, 2022 katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma ambapo Mgeni Rasmi wa Siku hiyo muhimu anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Jumanne Sagini (kulia) akipata maelezo kutoka kwenye banda la Jeshi la Polisi wakati alipotembelea Mabanda ya Wiki ya Sheria katika Viwanja vya Nyerere 'Square' jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Jumanne Sagini (kulia) akipata maelezo ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Uhamiaji kutoka kwa Afisa kutoka Ofisi hiyo.
Mkaguzi kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Bi. Ndekela Mwakipesile (kulia) akitoa maelezo ya majukumu mbalimbali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Jumanne Sagini wakati alipotembelea banda hilo.
Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Charles Magesa (kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu Maonesho ya Wiki ya Sheria kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Jumanne Sagini aliyetembelea Maonesho hayo jana tarehe 27 Januari, 2022.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama)
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment